TANGAZO


Friday, November 24, 2017

Emmerson Mnangangwa ndiye rais mpya wa Zimbabw

Wakulima watalipwa fidia - Mnangagwa

Rais mpya wa Zimbabwe amesema kuwa jukumu lake halitatekelezwa kupitia hutuba.
Lazima nianze kazi....
Tutaanza kazi kwa haraka kutoka pale alipowachia aliyekuwa rais wetu Robert Mugabe.
Hatuwezi kubadili yaliopita, kuna mengi ambayo tunaweza kufanya kwa sasa ili kulipatia taifa letu mwelekeo mpya.
Hatuwezi kukubali kuwa watumwa wa yaliopita.
Amesema kuwa mabadiliko ya umiliki wa ardhi yalifanyika na hayawezi kubadilishwa kwa kuwa huo utakuwa ukiukaji mkuu wa upiganiaji wa Uhuru.
Lakini rais huo mpya ameahidi kuwalipa wakulima waliopoteza mashamba yao katika sera tata iliotekelezwa na utawala wa rais MUgabe.

Rais Emmerson Mnangagwa ahutubia taifa

Emmerson Mnangagwa, kwa jina la utani The the crocodile", ameanza hotuba yake kama rais wa Zimbabwe.
''Nahisi furaha sana kwa uamuzi wa chama cha Zanu PF kunialika kuhudumia taifa letu la Zimbabwe kama rais na kamanda mkuu wa majeshi kuanzia leo''.
''Sina ujuzi wa kazi hii lakini nitawahudumia wananchi wote bila upendeleo wa rangi ama kabil''a. Amemsifu Robert Mugabe kwa kupiginia uhuru huku akisema kuwa alichukua uongozi wakati mgumu .
Amesema kuwa licha ya makosa yaliofanywa na Mugabe ni muhimu kukubali na kutambua mchango wake kuhusu ujenzi wa taifa. ''Kwangu mie bado ni rafiki mkubwa''.
Rais mpya wa Zimbabwe akiwahutubia raia
zbc
Rais mpya wa Zimbabwe akiwahutubia raia

Wakuu wa jeshi wampigia saluti Mnangagwa

Wakuu wa jeshi sasa wanampigia saluti kamanda mpya wa jeshi na kusalimiana kwa mkono.
Ni Jeshi lililochukua jukumu kuu siku 10 zilizopita ambazo zilisababisha kujiuzulu kwa Robert Mugabe.
Bwana Mnangagwa amesema kuwa amekuwa akiwasiliana na makamanda wakati alipofurushwa na rais Mugabe kama naibu wake.
Alisema kuwa kulikuwa na mpango wa kutaka kumuua ndio sababu akaondoka nchini humo na kurudi siku ya Jumatano baada ya Mugabe kujiuzulu.
Chiwenga
Reuters
Chiwenga

Rais Emmerson Mnangagwa akagua gwaride la jeshi

Akaunti moja ya mtandao wa twitter unaochunguza vyombo vya habari nchini Zimbabwe imesema kuwa rais mpya anakagua gwaride la heshima kwa kutembea huku aliyekuwa rais wa zamani Robert Mugabe mwenye umri wa miaka 93 alikuwa akifanya hivyo kwa kutumia gari.
Rais Emmerson Mnangagwa akagua gwaride la jeshi
Reuters
Rais Emmerson Mnangagwa akagua gwaride la jeshi

Mizinga 21 yapigwa kumakribisha rais mpya

Umati wa watu ulipiga kelele kufuatia hatua ya jeshi kupiga hewani risasi 21 kama heshima za kumkaribisha rais mpya
Mizinga 21 yapigwa kumakribisha rais mpya
ZBC
Mizinga 21 yapigwa kumkaribisha rais mpya

Mkewe rais Auxilia Mnangagwa ampiga busu mumewe

Umati uliohudhuria ulifurahia baada ya mkewe rais Auxilia Mnangagwa kumpiga busu mumewe
Mkewe rais Auxilia Mnangagwa ampiga busu mumewe
Reuters
Mkewe rais Auxilia Mnangagwa ampiga busu mumewe

Mnangagwa aapa kulinda haki za raia wa Zimbabwe

Raia wa Zimbabwe wamekusanyika kwa wingi kwenye uwanja wa michezo mjini katika mji mkuu wa nchi hiyo Harare kwa ajili ya sherehe za kuapishwa kwa rais mpya wa nchi hiyo Emmerson Mnangagwa.
Mnangagwa ameapishwa kama rais wa Zimbabwe, kufuatia kuondoka kwa rais kuondoka kwa Robert Mugabe madarakani baada ya miaka 37 ya utawala wa kiimla.
Makamu huyo wa zamani wa rais ambaye alirejea kutoka uhamishoni Jumatano -ameapishwa katika uwanja michezo wa Harare.
Kufutwa kwake kazi mwezi huu kulipelekea chama tawala cha Zanu-PF na jeshi kuingilia kati na kumlazimisha Mugabe ang'atuke .
Upinzani unamtaka Bwana Mnangagwa, ambae amekuwa mmoja wa watawala kumaliza "utamaduni wa ufisadi". Taarifa ya kuondoka madarakani kwa Mugabe mwenye umri wa miaka 93 hapo siku ya Jumanne iliibua sherehe kubwa kote nchini Zimbabwe.
Emmerson Mnangagwa akiapishwa
Reuters
Emmerson Mnangagwa akiapishwa

Kiapo cha Emmerson Mnangagwa

''Mimi Emmmerson Dambudzo Mnangagwa naapa kwamba kama rais wa jamhuri ya Zimbabwe nitakua muaminifu kwa Zimbabwe na kuheshimu na kuilinda katiba pamoja na sheria zengine zote za Zimbabwe na nitakuza chochote kitakachoeedeleza na nitapinga chochote kitakachoathiri Zimbabwe na nitalinda na kukuza haki za watu wa Zimbabwe na kwamba nitatekeleza majukumu yangu kwa nguvu zangu zote na uwezo wangu wote na nitaheshimu haki za Zimbabvwe na raia wake ,ewe mwenyezi mungu nisaidie''.
Rais mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnagangwa
Reuters
Rais mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnagangwa

HABARI ZA HIVI PUNDERais mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa aapishwa

Hatimaye rais mpya wa Zimbabwe Emmerson ameapishwa rasmi kuchukua wadhfa huo kufuatia kujiuzulu kwa Robert Mugabe aliyeliongoza taifa hilo kwa miaka 37 tangu taifa hilo lijipatie Uhuru
Emmerson Mnangagwa aapishwa kuwa rais wa Zimbabwe
reuters
Emmerson Mnangagwa aapishwa kuwa rais wa Zimbabwe

No comments:

Post a Comment