TANGAZO


Tuesday, October 17, 2017

KIKAO CHA BUNGE CHA KAMATI YA BUNGE YA MASUALA YA UKIMWI NA TAMISEMI

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI wakiwa katika Kikao na Waziri  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za  - TAMISEMI Mheshimiwa Selemani Jafo pamoja na watendaji wa Wizara  wakati walipopokea  na kujadili Taarifa kuhusu ufanisi wa utekelezaji wa mwongozo wa utumiaji na ugawaji wa fedha za UKIMWI kwenye Halmashauri za Miji na Manispaaa nchini.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI – Afya, Dkt Zaiba Chaula(aliyesimama) akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Bunge ya  Masuala ya Ukimwi wakati walipowasilisha Taarifa kuhusu ufanisi wa utekelezaji wa mwongozo wa utumiaji na ugawaji wa fedha za UKIMWI kwenye Halmashauri za Miji na Manispaaa nchini. Wakwanza kulia ni Waziri  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za  - TAMISEMI Mheshimiwa Selemani Jafo na wapili ni Naibu waziri wa wizara hiyo Mheshimiwa Josephat Kandege.  
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI Mheshimiwa Dkt. Jasmine Tisekwa  akisisitiza jambo baada ya kamati yake kupokea na kujadili Taarifa kuhusu ufanisi wa utekelezaji wa mwongozo wa utumiaji na ugawaji wa fedha za UKIMWI kwenye Hamlashauri za Miji na Manispaaa nchini. Kulia ni Mheshimiwa Osca Mukasa Mjumbe wa Kamati na kushoto ni Bi Happiness Ndalu Katibu wa kamati hiyo. 
Waziri  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mheshimiwa Selemani Jafo akijibu maswali ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI (hawapo pichani) katika kikao ambacho wizara yake iliwasilisha Taarifa kuhusu ufanisi wa utekelezaji wa mwongozo wa utumiaji na ugawaji wa fedha za UKIMWI kwenye Halmashauri za Miji na Manispaaa nchini.

No comments:

Post a Comment