TANGAZO


Thursday, July 6, 2017

TAMKO LA MAKATIBU WA WILAYA WA KANDA SITA ZA TANZANIA BARA WA CHAMA CHA WANANCHI (CUF)

THE CIVIC UNITED FRONT
     (CUF- Chama Cha Wananchi)
 
TAMKO LA MAKATIBU WA WILAYA WA KANDA SITA ZA TANZANIA BARA
KATIKA KIKAO KILICHOFANYIKA HAPA DODOMA – MAKAO MAKUU YA NCHI  KATIKA UKUMBI WA VIJANA SOCIAL LEO TAREHE 05/07/2017.
Waheshimiwa Wanahabari,
Waheshimiwa Viongozi wa CUF
Waheshimiwa Wanachama wa CUF – Chama Cha Wananchi
Naomba nianze kuwasalimu kwa salamu ya Chama chetu,
HAKI SAWA KWA WOTE
Awali ya yote tunatoa shukrani zetu za dhati kwa ujio wenu wa kuja kutusikiliza Tamko letu hili leo hii Tarahe 05/07/2017.
Maazimio ya Kikao cha Makatibu wa kanda sita za Tanzania Bara.
Tunatamka kwa pamoja kwamba:
1.      Ibrahim H. Lipumba hana ugomvi na Maalim Seif bali ana ugomvi na Chama Wananchi – CUF.  Wanachama wa Chama cha Wananchi – CUF wa Tanzania Bara hatumuungi mkono Prof. Lipumba kama anavyotangaza katika vyombo vya habari siyo kweli, bali ni muongo mzandiki mkubwa anataka kuionesha jamii ya Watanzania kuwa kuna chuki baina ya CUF Tanzania Bara na CUF Zanzibar, nasi tunafahamu kwamba kuwatenganisha Wazanzibar na Watanzania Bara ni  kuvunja Muungano, hivyo Prof. Lipumba ni adui mkubwa wa Muungano.
 
2.     Sisi Makatibu ambao tunawakilisha kanda sita za Tanzania Bara tunasikitika na kuhuzunishwa kwa kitendo cha Mkurugenzi wa RITA kuisajili Bodi ya Prof. Ibrahim Lipumba na genge lake kinyume kabisa na katiba yetu ya mwaka 1992 toleo la 2014, kifungu cha 98 (uk 90). . Ambacho kinaelezea Bodi ya Wadhamini ya chama cha CUF uteuliwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa ambalo linapatikana kwa mujibu wa Ibara 79 (1) (m) uk 69. Kikao kinawaagiza Wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa waliochaguliwa na Mkutano Mkuu wa Taifa kwa sharti la Katiba Ibara 79 (g) kumshitaki Mkurugenzi wa RITA kwa kitendo cha kushindwa kujiridhisha na kulitambua na kuyatambua maamuzi halali ya uteuzi uliofanywa na Baraza Kuu hilo halali ambalo ndilo lenye mamlaka ya kuteua wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya chama chetu CUF.
3.      Sisi Makatibu wa Wilaya za Kanda sita za Tanzania Bara, tutaendelea kulitambua Baraza Kuu la Uongozi Taifa lililochaguliwa Juni 2014 kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza Dar es Salaam.
4.      Sisi Makatibu wa Wilaya wa kanda Sita tunamtaka Ibrahim Lipumba atuachie Ofisi yetu (Ofisi Kuu) iliyopo Buguruni Dar es Salaam mara moja na akaombe ajira kwa msajili wa vyama vya siasa ili ampangie kazi nyengine, kama akiendelea kukaidi sisi wanachama tutakuja kuchukua ofisi yetu wenyewe mara moja.
5.      Sisi Makatibu sita tunalipongeza Baraza Kuu la Uongozi la Taifa chini ya Jemedari wetu Katibu Mkuu wetu Mhe, Maalim Seif Sharif Hamad kwa juhudi wanazochukua kunusuru chama chetu kwa kukitoa kwenye makucha ya Kibaraka Ibrahim Lipumba pamoja na genge lake.
6.      Mwisho tunawakumbusha Makatibu Wote wa Wilaya kuandika taarifa zote za chama na kuzielekeza Makao Makuu ya chama ambapo katiba yetu inaelekeza kwa muibu wa ibara 123 na Tunanukuu “Mwenyekiti Taifa, Makamu Mwenyekiti Taifa, Katibu Mkuu, Manaibu Katibu Mkuu, Wakurugenzi na Manaibu Wakurugenzi wa Chama watakuwa na Ofisi zao Makao Makuu ya chama na, au Ofisi Kuu ya chama, lakini kiongozi yoyote aliyetajwa katika kifungu hiki anaweza kufungua Ofisi ya muda au kudumu katika sehemu nyingine ya nchi pindi akipata idhini ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa.”.
Naomba kuwasilisha.
Ally A. Darema
Kwa Niaba ya Makatibu wa Kanda Sita.
 

No comments:

Post a Comment