TANGAZO


Thursday, July 20, 2017

Nkurunziza afika Tanzania ziara yake ya kwanza nje tangu 2015

Nkurunziza na Magufuli

Haki miliki ya pichaIKULU, TANZANIA
Image captionRais Nkurunziza akiwa na mwenyeji wake Rais John Magufuli baada ya kufika Ngara, kaskazini magharibi mwa Tanzania
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza anafanya ziara yake ya kwanza ya kigeni tangu kufeli kwa jaribio la kupindua serikali yake zaidi ya miaka miwili iliyopita.
Amesafiri na mawaziri kadha kwenda nchini Tanzania, ambao imetoa makao kwa zaidi ya wakimbizi robo milioni kutoka Burundi.
Watu hao waliikimbia Burundi baada ya mzozo uliotokana na hatua ya Bw Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.
Nkurunziza alikuwa akihudhuria mkutano nchini Tanzania wakati jaribo hilo lilipofanyika mwezi Mei mwaka 2015.
Mamia ya watu wameuawa tangu mzozo huo uanze wengi wanaodaiwa kuwa wafuasi wa upinzani.
Mamia ya watu wameuawa tangu mzozo huo uanze wengi wanaodaiwa kuwa wafuasi wa upinzani.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionMamia ya watu wameuawa tangu mzozo huo uanze wengi wanaodaiwa kuwa wafuasi wa upinzani.
Magufuli na NkurunzizaHaki miliki ya pichaIKULU, TANZANIA

No comments:

Post a Comment