Kiongozi wa upinzani nchini Zambia aliye korokoroni Hakainde Hichilema, amefikisha siku 100 gerazani tangu akamatwe akilalamikia mazingira mabaya yaliyo gerezani.
Alikamatwa baada ya msafara wake kukataa kuupisha ule wa rais
Anakabiliwa na mashtaka uhaini kufuatia kisa hicho.
- Kinara wa upinzani nchini Zambia azuia msafara wa Rais
- Kiongozi wa upinzani Zambia afunguliwa mashtaka ya uhaini
- Kiongozi wa upinzani Zambia Hichilema ashtakiwa
Bwana Hichilema ambaye kwa sasa anazuiliwa katika gereza lenye ulinzi mkali, aliandika kwenye mtandao wake wa Facebook kuwa hana chuki na yeyote
Alisema mapenzi yake ni kuona mabadilko nchini Zambia.
"Tunaamini kuwa licha ya wafungwa hawa kufanya makosa, wanahitaji kuhudumiwa kwa njia ya kibinadamu," alisema hichilema.


No comments:
Post a Comment