TANGAZO


Tuesday, June 13, 2017

WIZARA YA ARDHI WAFANYA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI JUU YA TATHMINI YA ULIPAJI WA KODI YA PANGO LA ARDHI NA MALIPO YAKE KWA MFUMO MPYA WA KIELEKTRONIKI

Kamishna Msaidizi wa Ardhi, Kanda ya Kati Bw. Hezekiely Kitilya akiwa katika mkutano na waandishi wa habari, akizungumzia tathmini ya ulipaji kodi ya pango la ardhi na Malipo yake yanavyo weza kufanyika kwa mfumo mpya wa kielektroniki leo, mjini Dodoma. 
Afisa Ardhi Mwandamizi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bi.Jane Kapongo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu Hati za Kimila kutumika kama dhamana katika Taasisi za Kifedha nchini leo, Mjini Dodoma. 
Msajili wa Hati kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw.Geofrey Mauya akizungumza na waandishi wa habari juu ya taratibu mbalimbali za hati na jinsi ya kuzipata katika mkutano na waandishi wa habari, Mjini Dodoma leo. 
Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Kati Bw. Hezekiely Kitilya, akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari juu ya tathmini ya ulipaji kodi ya pango la ardhi na Malipo yake yanavyoweza kufanyika kwa mfumo mpya wa kielektroniki leo, mjini Dodoma.(Picha zote na Daudi Manongi-Maelezo, Dodoma)

No comments:

Post a Comment