TANGAZO


Monday, June 19, 2017

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA UZINDUZI WA KAMUSI KUU YA KISWAHILI BUNGENI MJINI DODOMA LEO

Waziri Mkuu  Mhe. Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua kamusi kuu mpya ya Kiswahili leo Mjini Dodoma.Kushoto ni Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu na kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Mhe. Dk. Harrison Mwakyembe. (Picha zote na Daudi Manongi-Maelezo, Dodoma)
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akionyesha Kamusi Kuu Mpya ya Kiswahili kwa Wabunge mara baada ya kuizindua leo Bungeni Mjini Dodoma. 
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akipokea Kamusi kuu mpya ya Kiswahili kutoka kwa Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu mara baada ya kuizindua leo Bungeni. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza jambo na Mbunge wa Kuchaguliwa na Balozi wa Lugha ya Kiswahili Afrika, Mhe. Salma Kikwete na Naibu Waziri wake mara baada ya uzinduzi wa Kamusi kuu mpya ya Kiswahili Bungeni Mjini Dodoma leo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dk. Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi waandamizi wa Wizara yake na wachapishaji wa Kamusi hiyo (Longhorn Publisher) na wageni wengine waliohudhuria uzinduzi huo leo Mjini Dodoma.  

No comments:

Post a Comment