TANGAZO


Monday, December 12, 2016

Rwanda kufanya uchaguzi wa rais Agosti, 2017

Paul KagameImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionKwa mujibu wa katiba mpya ya rais Paul Kagame anaruhusiwa kuwania muhula wa tatu.
Serikali ya Rwanda imetangaza tarehe za uchaguzi wa rais unaotarajiwa kufanyika mwakani.
Kulingana na tangazo la lililotolewa baada ya kikao cha baraza la mawaziri uchaguzi huo utafanyika tarehe 4 Agosti, 2017.
Shughuli za kampeni zitaanza mwezi Julai lakini hakuna tarehe rasmi iliyotangazwa kwa wagombea kuwasilisha hati za kugombea urais, licha ya kwamba tangazo hilo linasema wagombea watatangazwa kabla ya kuanza kwa kampeni.
Kwa mujibu wa katiba mpya ya rais Paul Kagame anaruhusiwa kuwania muhula wa tatu.
Mtu pekee katika kambi ya upinzani aliyetangaza nia yake ya kugombea urais ni kasisi wa zamani wa kikatoliki Joseph Nahimana. Hata hivyo juhudi zake za kutaka kurejea nchini Rwanda wiki mbili zilizopita ili kuandikisha chama chake na kugombea urais ziligonga mwamba.
Kasisi Joseph Nahimana na wenzake watatu walikataliwa kuingia nchini Rwanda walipokuwa mjini Nairobi Kenya kuelekea Rwanda kutoka nchini Ufaransa anakoishi kama mkimbizi.
Serikali ya Rwanda haikutaka kuzungumza lolote kuhusu tukio hilo, lakini mashirika ya Rwanda yanayotetea maslahi ya manusura wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 walikuwa wameanza kulalamika kuwa tovuti ya Padre Nahimana akamatwe kwa madai kwamba tovuti yake inaendeza na kuchoche fikra za mauaji ya kimbari.

No comments:

Post a Comment