TANGAZO


Sunday, December 11, 2016

NAPE: WADAU JITOKEZENI KUDHAMINI TUZO ZA MUZIKI NA FILAMU NCHINI


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwasalimia baadhi ya mashabiki waliofika kuhudhulia sherehe za Tuzo za Filamu na Muziki za EATV 2016 zilizofanyika Desemba 10, 2016 Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na watangazaji wa EATV mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Mlimani City kuhudhulia hafla ya tuzo za Filamu na Muziki za EATV zilizofanyika Desemba 10, 2016 Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati) akifuatilia burudani mbalimbali kutoka kwa  wasanii wa ndani na nje ya nchi wakati wa hafla ya tuzo za Filamu na Muziki za EATV zilizofanyika Desemba 10, 2016 Jijini Dar es Salaam.








Baadhi ya wasanii wa muziki wakitoa burudani katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanamuziki na wasanii wa Filamu(EATV Awards 2016) zilizofanyika Desemba 10, 2016 Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa wanamuziki na wasanii wa Filamu(EATV Awards 2016) zilizofanyika Desemba 10, 2016 Jijini Dar es Salaam.


Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa(BASATA) Bw. Godfrey Muingereza akitoa wito kwawadau kuendelea kushirikiana na BASATA kufanikisha Tuzo mbalimbali nchini katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanamuziki na wasanii wa Filamu(EATV Awards 2016) zilizofanyika Desemba 10, 2016 Jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi wa Bodi ya Filamu Tanzania Bw. Romanus Tairo akitoa rai kwa wasanii wa Filamu nchini kufata sheria na taratibu za uandaaji na usambazaji wa filamu zao nchini katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanamuziki na wasanii wa Filamu(EATV Awards 2016) zilizofanyika Desemba 10, 2016 Jijini Dar es Salaam.



Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akitoa tuzo ya heshima kwa Bw. Bonny Kilosa(Dj Bonny Love) kwa machango wake katika tasnia ya muziki nchini katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanamuziki na wasanii wa Filamu(EATV Awards 2016) zilizofanyika Desemba 10, 2016 Jijini Dar es Salaam.


Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Muingereza akitoa tuzo kwa Msanii Ali Kiba ambaye alichukua Tuzo tatu ikiwemo Wimbo Bora wa Mwaka, Msanii Bora wa Kiume na Video Bora ya Mwaka.


Mwakilishi wa Bodi ya Filamu Tanzania Bw. Romanus Tairo akitoa tuzo kwa mshindi wa Filamu Bora ya Mwaka ya Safari ya Gwalu Bw. Gabo Zigamba.





Baadhi ya mashabiki wa Muziki na filamu wakifuatilia burudani mbalimbali katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanamuziki na wasanii wa Filamu(EATV Awards 2016) zilizofanyika Desemba 10, 2016 Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa tuzo za Muziki na Filamu EATV 2016.(Picha/Habari na Raymond Mushumbusi)

WADAU wa Sanaa nchini wameshauriwa kujitokeza kudhamini tuzo kwa ajili ya wasanii wa muziki na filamu nchini ili kuendelea kuzipa nguvu tasnia hizo kwa maendeleo yake.


Ushauri huo umetolea jana na wazori wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo kwa wasanii wa muziki na Filamu nchini zilizoandaliwa na kituo cha Televisheni cha East Africa (Channel 5).

Ameongeza kuwa wadhamini wengi wajitokeze kwa  ili kuongeza idadi ya tuzo zenye kiwango kinachostahili zenye kuzingatia weledi na usawa katika utoaji wake.

“Niwaombe wadau wa sanaa nchini jitokezeeni kudhamini tuzo hizi za filamu na Muziki ili tuwe na tuzo nyingi zaidi na zenye viwango vya kimataifa”Alisistiza Mhe. Nnauye.

Kwa upande wake katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Muingereza amesema kuwa BASATA itaendelea kushirikiana na wasanii na wadau wa Sanaa katika kuandaa na kusimamia tuzo mbalimbali ikiwa ni nia ya Serikali kuikuza tasnia ya muziki na filamu ambayo ni moja ya tasnia inayoajiri vijana wengi kwa sasa.

“Nawaalika wadau wa Sanaa na wasanii wote sisi tuko tayari kushirikiana nao katika kulisukuma hili guruduma la maendeleo ya Sanaa nchini na nawasahuri tufate tu utaratibu katiaka kuandaa kazi zenu za sanaa” alisema Bw. Muingereza.

Aidha mwakilishi wa Bodi ya Filamu Tanzania Bw.Romanus Tairo amesisitiza wasanii wa filamu nchini kufata sheria na gtaratibu zote kabla ya kuandaa na kusambaza filamu zao.

“Nawaomba wasanii wote wa filamu nchini kufuata Sheria na taratibu zilizopo za kusajili filamu zote zikakaguliwa na kuoewa kibali cha kuoneshwa sehemu mbalimbali”Alisema Bw.Tairo.

Tuzo za Muziki na Filamu za EATV zimeanzishwa kwa dhumuni la kuongeza chachu ya maendeleo ya tasnia ya muziki na filamu nchini na jumla ya tuzo nane zilitolewa kwa wasanii wa muziki na filamu na tuzo moja ya heshima ilitolewa kwa msanii aliyetoa mchango mkubwa katika tasnia ya muziki nchini Bw. Bonny Kilosa (Dj Bonny Love).
 

No comments:

Post a Comment