Mlipuko kwenye kanisa moja la wakristo wa Coptic karibu na mji wa Cairo nchini Misri, limewaua takriban watu 20.
Televisheni moja nchini Misri inasema kwa watu 22 wameuawa na wenegine 35 kujeruhiwa kwa mujibu wa maafisa wa wizara ya afya.
Vyombo vya habari vya Misri vilisema kuwa mlipuko huo ulotokea kwenye kanisa na St Peters.
Kilichosababisha mlipuko huo bado hakijulikani.
Mlipuko huo ulitokea mwendo wa saa nne saa za Misri,
Wakirsto Coptic nchini Misri huchukua karibu asilimia 10 ya watu wote nchini humo.
Kanisa St Mark's Cathedral ni makao makuu ya kanisa ki-othodox la wakristo nchini Misri na makao makuu ya kinara wake mkuu wa kidini Papa Tawadros wa Pili.
No comments:
Post a Comment