Mikononi mwa daktari kichwa cha mtoto Ibrahim kinaonekana kidogo mno. Anamshika mtoto huyo taratibu kwa uangalifu. Kila kitu kando yake kinaokena kikubwa.
Nepi ambazo amevalishwa ndizo ndogo zaidi zinazopatikana lakini bado ni kubwa mno kwake. Anaonekana kuwa na macho makubwa, mbavu zake zikionekana kusukuma nje ya mwili wake
Ni vigumu kumtaja mtoto aliye katika hali hii kuwa aliye na bahati. Lakini Ibrahimu ameishi siku 21 na madaktari wana matumaini kuwa ataishi. nduguye yake waliozaliwa pamoja alikufa baada ya kuzaliwa.
Mamake Wafaa Hatem, ameketi kitandani kando yake, akimtuliza anapolia.
Sawa na raia wengine milioni 3 nchini Yemen , familia hiyo ililazimika kuhama kwao kutokana na vita. Changamoto zao za kila siku ni kupata chakula.
Babake Ibrahimu ni dereva wa teksi, lakini hali mbaya ya uchumi imekuwa changamoto kubwa kwake kupata wateja
Ni moja ya shuhuda kutoka kwa vita ambavyo vimesababisha viwango vya utapiamlo kupanda kwa asilimia 200 katika kipindi cha miaka miwili.
Asilimia 50 ya hospitali hazifanyi kazi. Zingine zimeshambuliwa na muungano unaoongozwa na Saudi Arabia na zingine zimefungwa kwa kukosa ufadhili.
Usafirishaji wa misaada mara nyingine huzuiwa na waasi ambao wanataka kudhibiti shughuli hiyo. wafanyakazi wengi wakiwemo walio kwenye sekta ya afya hawajalipwa kwa takriban miezi minne.
Mashirika kama vile la madaktari wasio na mipaka wanajaribu kusaidia lakini majukumu ni mazito.
Mfumo wote umeporomoka, hospitali zinafungwa mara kwa mara. Kwa hivyo ni jambo la kutia wasi wasi kuona nchi hii ambayo tayari ilikuwa imethiriwa na umaskini na uongozi mbaya inazama kila siku.
Ukitembea kwenye viumba vya hospitali picha kamilki ya vita inaonekana.
Unaona wakulima ambao walikuwa wakienda sokoni wakiwa na majeraha na mabomu ya mashambulizi ya ndege za Saudi Arabia huku watoto wakiugua kutokana na utapia mlo.
Vijijini , waliko watu maskini wasio na uwezo wa kusafiri kwenda hosptalini, hukaribia wageni wakiwa na matumaini kuwa huenda wamekuja na misaada.
Mwanamme moja mzee ambaye haombi chakula, anatizama akiwa amawakusanya wajukuu wake wanne walio na njaa.
Wafanyakazi kutoka shirika la Save the Children, husimamia zaanati za afya eneo hilo lakini mara nyinig hulemewa na mahitaji makubwa.
Ukosefu wa maji safi ya kunywa umesababisha mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.
Hali iliyo nchini Yemen imegubikwa na vita vilivyo nchini Syria na Iraq.
No comments:
Post a Comment