TANGAZO


Tuesday, October 11, 2016

Wenye Samsung Galaxy Note 7 watakiwa kuzizima

Samsung battery fire

Image copyrightREUTERS
Image captionSimu ya Samsung Note 7 ilishika moto ikifanyiwa uchunguzi maabarani Singapore
Samsung imetoa wito kwa watu wenye simu aina ya Galaxy Note 7 kuzizima mara moja huku ikifanya uchunguzi kubaini ni kwa nini simu hizo, hata zile ambazo kampuni hiyo ilikuwa imethibitisha kwamba ni salama, zinawaka moto.
Kampuni hiyo ya Korea Kusini imesema itasitisha uuzaji wote wa simu hizo.
Samsung iliwataka watu waliokuwa wamenunua jumla ya simu 2.5 milioni mwezi Septemba kuzirejesha madukani baada ya wateja wengi kulalamika kwamba betri za simu hizo zilikuwa zinalipuka.
Walipewa simu mpya ambazo zilidaiwa kuwa salama.
Lakini sasa taarifa zimetokea kwamba hata simu hizo zilizodaiwa kuwa salama zinashika moto.
Mwanamume mmoja jimbo la Kentucky, Marekani anasema aliamka na kupata chumba chake cha kulala kimejaa moshi uliotokana na simu mpya ya Note 7 aliyokuwa ameipata baada ya kurejesha ya awali.
Siku chache awali, abiria kwenye ndege moja Marekani walitakiwa kuondoka kwa dharura ndegeni baada ya simu ya Note 7 kuanza kutoa moshi.
Galaxy Note 7 in South KoreaImage copyrightAFP
Image captionSamsung imesitisha mauzo ya Galaxy Note 7
"Kwa sababu usalama wa wateja ni jambo tunalotilia maanani zaidi, Samsung itawataka wasambazaji wote na wauzaji wake kote duniani kusitisha uuzaji na pia ubadilishaji wa simu za Galaxy Note 7 uchunguzi unapoendelea," kampuni hiyo imesema.
"Wateja walio na simu asili za Galaxy Note 7 au simu za Galaxy Note 7 za kubadilisha, wanafaa kuzizima na kuacha kuzitumia na badala yake kutumia njia nyingine (kuendelea na shughuli zao)," kampuni hiyo imeongeza.

Ni watu wangapi wameathirika?

Samsung inasema simu zilizoathirika ni takriban 2.5 milioni. Kwa mujibu wa kampuni hiyo, simu 45,000 za Note 7 zimeuzwa Ulaya, na sana Uingereza. Zaidi ya asilimia 75 zilikuwa zimebadilishwa na wamiliki wake wakapewa simu nyingine za Note 7 au mitambo mingine ya Samsung.
Samsung sasa itashindwa na Apple?
Galaxy Note 7 ilitarajiwa na Samsung kuisaidia kushindana na simu ya Apple iPhone 7. Lakini baada ya matatizo hayo, Samsung imeathirika pakubwa na hisa zake kushuka. Hisa za Apple upande mwingine zimepanda sana thamani. Aidha, nembo ya Samsung kama kampuni ya kuaminika imeathirika pakubwa.
Wakala wa kulinda wateja Marekani amewahimiza watu kutotumia simu za Samsung ambazo wamebadilishiwa.
Mwenyekiti wa usalama katika tume hiyo ya Elliot Kaye amesema uamuzi wa Samsung wa kuacha kuuza simu hizo ni wa busara.

No comments:

Post a Comment