TANGAZO


Thursday, October 6, 2016

Wanasayansi wa Urusi wasema Crimea inahama na 'kuelekea Urusi'

NASA satellite image of the Crimean peninsula

Image copyrightNASA
Image captionRasi ya Crimea inasonga asteaste kaskazini mashariki, wanasayansi wa Urusi wamesema
Wanasayansi kutoka nchini Urusi wanasema eneo la Crimea ambalo limekuwa likizozaniwa linasonga milimita kadha kila mwaka kuelekea Urusi.
Wanakadiria kwamba rasi hiyo ya Crimea itafikia Urusi katika kipindi cha miaka 1.5 milioni ijayo.
Kwa mujibu wa Alexander Ipatov, anayeongoza taasisi ya anga za juu na sayansi nchini Urusi, rasi hiyo ambayo ilitwaliwa na Urusi kutoka Ukraine mwaka 2014 inasonga kaskazini mashariki kwa kasi ya milimita 2.9 kila mwaka, shirika la Interfax limeripoti.
"Crimea ilipojiunga na Urusi, tulianza kujiuliza Crimea inaelekea wapi. Tumebaini kwamba inasonga kuelekea Urusi," Ipatov anasema.
Anaongeza kwamba ingawa huenda hilo likaonekana kama mzaha, hayo ni matokeo ya utafiti wa makini sana.
Walifanya utafiti huo kupima ardhi ya Crimea kwa vifaa vya kisayansi vilivyowekwa kisiwa cha Simeiz kwenye ras hiyo kwa mujibu wa Interfax.
Kufuatia kutangazwa kwa habari hizo, baadhi ya Warusi mtandaoni wameanza kufanya mzaha wakisema sasa Urusi haitakuwa na haja ya kujenga daraja la juu kwa juu la kuunganisha Crimea na Urusi bara.
Daraja hilo la Kerch la urefu wa 19km (11.8 mile) linaendelea kujengwa, na linatarajiwa kugharimu $3.5bn (£2.75bn).
Mwaka 2007, mtaalamu mwingine wa jiolojia Boris Levin alisema eneo jingine linalozozaniwa, visiwa vya Kuril, vinasonga kuelekea visiwa vya Urusi vya Sakhalin kwa kasi ya mililita 18 kwa mwaka, gazeti linaloegemea upande wa serikali la Izvestia liliripoti.
Daraja Kerch la kuunganisha Urusi na Crimea
Image captionDaraja Kerch la kuunganisha Urusi na Crimea linaendelea kujengwa

No comments:

Post a Comment