TANGAZO


Tuesday, October 11, 2016

Wanajeshi wa Ethiopia waondoka kambi muhimu Somalia

Wanajeshi wa Ethiopia waliingia nchini Somalia kuisaida serikali dhaifu ya nchi hiyo

Image copyrightAFP
Image captionWanajeshi wa Ethiopia waliingia nchini Somalia kuisaida serikali dhaifu ya nchi hiyo
Wanajeshi wa Ethiopia wanaopigana vita na kundi la wanamgambo wa al-Shabab nchini Somalia ,wameondoka kutoka kambi yao muhimu kati kati mwa nchi hiyo katika eneo la Hiran.
Kwa sasa wapiganaji wa Al-Shabab wameingia kijiji cha el-Ali kufuatia kuondoka kwa wanajeshi hao wa Ethiopia.
Wanajeshi hao waliharibu kambi hiyo kabla ya kuondoka kwa mjibu wa kituo cha radio kinachomilikiwa na al-Shabab.
Sababu ya wanajeshi hao kuondoka bado haijulikani lakini al-Shabab walisema kuwa walishambulia kambi hiyo hivi majuzi.
Mwezi Juni al-Shabab walisema kuwa waliwaua wanajeshi 60 wa Ethiopia waliposhambulia kambi yao kweye mji wa Halgan kati kati mwa Somalia.
Baadhi ya wanajeshi wa Ethiopia wako nchini Somalia kama sehemu ya kikosi cha Muungano wa Afrika (AU).
Wanajeshi wa Ethiopia miongoni mwa wanajehsi 22,000 wa AU, wana jukumu la kulinda maeneo ya Bay, Bakool na Gedo na pia wako eneo la Hiram lililo karibu na mpaka wa Ethiopia.

No comments:

Post a Comment