TANGAZO


Tuesday, October 4, 2016

Wakamatwa Malaysia kwa kuvua nguo hadharani

Watalii 9 wa Australia wanachunguzwa Malaysia kwa utovu wa nidhamu

Image copyrightNIK ASYRAAF/@NIKASYRAAF
Image captionWatalii 9 wa Australia wanachunguzwa Malaysia kwa kuvua nguo hadharani
Watalii 9 kutoka Australia wamekamatwa baada ya kuvuwa nguo hadharani na kusalia na chupi wakati wa mashindano ya magari ya Grand Prix yaliofanyika Jumapili Malaysia.
Wanaume hao waliovalia chupi za bendera ya Malaysia wanachunguzwa kwa kutusi makusudi na pia uwezekano wa kushtakiwa kwa kuvuruga amani.
Picha za wanaume hao zilisambazwa katika mitandao ya kijamii.
Tukio hilo limeshutumiwa katika nchi hiyo yenye idadi kubwa ya waumini wa kiislamu.
Watumiaji mtandao wa Twitter wamewashutumu wanaume hao walio na umri wa kati ya miaka 25 na 29, kwa kulitusi taifa la Malaysia.
"Hamuwezi kuwa na heshima kidogo kwa taifa munalolitembelea?" ameandika @johnqgoh, huku wengine wakitaja hatua hiyo kama ya 'aibu na ujinga'.
Raia hao wa Australia wamezuiwa saa kumi na moja jioni Jumapili na watazuiwa kwa siku nne nje ya mji mkuu Kuala Lumpur, Mkuu wa polisi Sepang, Abdul Aziz Ali ameambia vyombo vya habari nchini.
Wanachunguzwa kwa kutoheshimu bendera ya taifa na kuvua nguo hadharani.
Malaysia ina sheria kali kuhusu kuzunguka uchi na raia wa mataifa ya nje wanaofanya makosa, hutozwa faini kabla ya kurudishwa nchi wanazotoka.
Mwaka jana mwanamke mmoja raia wa Uingereza alifungwa gerezani kwa kuvua nguo hadharani na kupiga picha juu ya mlima Kinabalu Malaysia.
Eleanor Hawkins, mwenye umri wa 23, alikiri kuvuwa nguo hadharani pamoja na watalii wengine watatu wa maatifa ya magharibi na alifungwa kwa siku tatu.

No comments:

Post a Comment