TANGAZO


Friday, October 7, 2016

WADA: IOC ilishindwa kuzuia wanariadha kutumia dawa za kusisimua misuli

WADA imesema OIC ilianza kupoteza mwelekeo kabla hata ya michuano hiyo kuanza

Image captionWADA imesema OIC ilianza kupoteza mwelekeo kabla hata ya michuano hiyo kuanza
Kamati ya kimataifa ya Olimpiki OIC imelaumiwa kwa kushindwa kuhakikisha wanariadha walioshiriki michuano ya Rio mwaka huu walikuwa hawatumii dawa zilizokataliwa michezoni.
Taarifa ya wakala wa kupambana na dawa hizo ulimwenguni WADA imesema OIC ilianza kupoteza mwelekeo kabla hata ya michuano hiyo kuanza.
Wanariadha walemavu kutoka Urusi hawakushiriki kabisa michuano ya Paralimpiki
Image captionWanariadha walemavu kutoka Urusi hawakushiriki kabisa michuano ya Paralimpiki
Taarifa hii imekuja baada ya OIC kuifungia Urusi na kisha kuifungulia kushiriki michuano ya Rio huku WADA wakiamini hawakustahili kufanya hivyo.
Zaidi ya wanaridha 270 wa Urusi waliruhusiwa kushiriki michuano hiyo baada ya kukata rufaa.
Hata hivyo kamati ya kimataifa ya Paralimpiki (IPC) iliwazuia wanamichezo wa Urusi kushiriki michuano ya Rio 2016.

No comments:

Post a Comment