TANGAZO


Tuesday, October 4, 2016

Waandamanaji Ethiopia wakishambulia kiwanda cha Dangote

Maandamano ya jamii ya Oromo

Image copyrightREUTERS
Kiwanda cha kutengeneza simiti kinachomilikiwa na tajiri wa Afrika, mfanyabiashara wa Nigeria Aliko Dangote, kimeshambuliwa na waandamanaji katika eneo la Oromia, utawala wa eneo hilo umesema katika taarifa yake.
Maandamano hayo yanafuta vifo vya watu 55 wakati kulizuka mkanyagano katika tamasha la dini la kabila la Oromo Jumapili.
Waandamanji wameteketeza magari na mashini katika kiwanda cha Dangote Cement Factory huko Ada Berga, shirika la habari la serikali Fana linaripoti.
Mtandao wa Amharic unaounga mkono upinzani , ZeHabesha.com, pia umeaangazia taarifa hiyo:
Mtandao wa ZeHabesha.comImage copyrightZEHABESHA.COM
Waandamanaji pia wanatuhumiwa kuwaachia huru wafungwa baada ya kutekez kituo cha polisi katika eneo la Bule Hora, FBC inaripoti.
Mahakama na magari ya serikali pia yameteketezwa, linaongeza.
Wanaharakati wanasema vikosi vya usalama vilifyetua risasi katika tamasha hilo, na kusababisha mkanyagano huo.
Tamasha hilo limekabiliwa na maandamano ya watu walioimba wakidai uhuru wa kisiasa Ethiopia.
Serikali imekana kuwa vikosi vya usalama vilifyetua risasi, na bada yake imeshutumu ghasia hizo kutukelezwa na 'watu waovu'.

No comments:

Post a Comment