TANGAZO


Saturday, October 1, 2016

Urusi yaionya Marekani na kuitaka isiishambulie Syria

Mji wa Aleppo umekuwa ukishambuliwa mara kadha

Image captionMji wa Aleppo umekuwa ukishambuliwa mara kadha
Urusi imeionya Marekani isichukue hatua yoyote ya kijeshi, dhidi ya wanajeshi wa serikali ya Syria.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje mjini Moscow, alieleza kwamba kuingilia kati kwa namna hiyo, kutasababisha yale aliyoeleza kuwa matokeo yatayotikisa Mashariki ya Kati nzima.
Marekani inamtaka Rais Assad aondoke madarakaniImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionMarekani inamtaka Rais Assad aondoke madarakani
Alisema, iwapo mshirika wa Urusi nchini Syria, Rais Bashar al-Assad, atatolewa madarakani, kutafuata pengo, ambalo haraka, litajazwa na magaidi.
Matamshi hayo yametolewa wakati wa mvutano mkubwa baina ya Urusi na Marekani, kuhusu mashambulio ya mabomu yanayoendelea, dhidi ya Aleppo.

No comments:

Post a Comment