TANGAZO


Monday, October 3, 2016

Upinzani wasusia serikali ya umoja Gabon

Waziri mkuu wa Gabon Emaniel Issozet Ngondet alishindwa kutengeza serikali ya umoja


Image copyrightAFP
Image captionWaziri mkuu wa Gabon Emaniel Issozet Ngondet alishindwa kutengeza serikali ya umoja

Upinzani nchini Gabon umefuata ahadi yake ya kususia serikali ya umoja iliopendekezwa na rais Ali Bongo.
Kutokana na hatua hiyo baraza hilo la mawaziri lenye wanachama 40 lililozinduliwa wikendi iliopita na waziri mkuu Emmaniel Issozet Ngondet lina mwanachama mmoja pekee wa upinzani Bruno Ben Moubamba.
Bwana Moubamba , ambaye hana umaarufu mkubwa alipata chini ya asilimia moja ya kura zote mnamo mwezi Agosti wakati wa uchaguzi huo wa urais uliokumbwa na utata.
Kiongozi wa upinzani Jean Ping,ambaye amekataa ushindi wa Bongo amekata kushirikishwa katika serikali.
Rais Bongo alimshinda Jean Ping kwa chini ya kura 6,000.
Hatahivyo kushirikishwa kwa Moubamba katika serikali mpya kunaonekana kuwa pigo kwa upinzani ambao unaonekana hauna umoja ukilinganisha na hapo awali.

No comments:

Post a Comment