TANGAZO


Friday, October 7, 2016

UNICEF: Wasichana hufanya asilimia 40 ya kazi za nyumbani

Wasichana hupata kazi nyingi za nyumbani wamewekewa kuzifanya wanapokuwa wakumbwa

Image copyrightUNICEF
Image captionWasichana hupata kazi nyingi za nyumbani wamewekewa kuzifanya wanapokuwa wakumbwa
Wasichana hutumia asilimia 40 ya wakati wao mwingi kufanya kazi za nyumbani ambazo hawalipwi ikilinganishwa na wavulana kulingana na ripoti mpya ya kitengo cha watoto katika shirika la Umoja wa Mataifa.
UNICEF imesema kuwa tofauti hiyo ya wakati uliotumika ni sawa na saa milioni 160 za ziada kwa siku.
Wawili kati ya wasichana watatu wanapika na kuosha nguo katika nyumba zao na nusu ya idadi hiyo hubeba maji na kutafuta kuni.
Pia hufanya kazi za uyaya mbali na kuwaangalia wazee,ripoti hiyo imesema.
Ripoti hiyo pia imebaini kwamba kazi za ziada huongezeka kwa wakati:kati ya umri wa miaka 5 na 9,wasichana hutumia muda wao mwingi kufanya kazi za nyumbani wafikiapo na kazi hizo huongezeka kwa asilimia 50 wafikiapo umri wa miaka 14.
Kazi kama vile kutafuta maji ama kuni zinaweza kuwaweka wasichana wadogo katika hatari ya unyanyasaji wa kingono,ripoti hiyo inasema.
Nchini Somalia ,wasichana walio kati ya umri wa miaka 10 na 14 hutumia saa 26 kwa wiki kufanya kazi za nyumbani,ikiwa, ni saa nyingi zaidi ikilinganishwa na taifa lolote jingine.
Burkina Faso na Yemen pia zina tofauti kubwa ya saa za kazi zinazofanywa kati ya wasichana na wavulana.

No comments:

Post a Comment