Mchezaji wa zamani wa timu ya soka ya Cameroon Rigobert Song amesafirishwa nchini Ufaransa ili kupata matibabu zaidi baada ya kupata fahamu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 40 alilazwa katika hospitali ya Younde siku ya Jumapili baada ya kupoteza fahamu.
Siku ya Jumanne aliwapungia mkono mashabiki nje ya kituo hicho cha matibabu alipokuwa akipelekwa katika uwanja wa ndege.
Mkurugenzi wa kituo hicho Daktari Louis Joss Bitang A Mafok amesema kuwa Song alitokwa na damu katika ubongo.
Nduguye Song Alexandre amefurahishwa na raia wa Cameroon kwa kumuombea Song afya njema.
''Wakati huu,familia yangu inaisha kwa matatizo.tumefurahishwa na mapenzi na usaidizi wa raia wa Camroon na kwengineko.,alisema.
Waziri wa afya nchini Cameroon Andre Mama Fouda pia alitoa usaidizi wake.
No comments:
Post a Comment