TANGAZO


Monday, October 3, 2016

Rigobert Song alazwa hospitalini Cameroon

Rigobert Song

Image copyrightGETTY IMAGES
Image captionSong alicheza Kombe la Dunia 1994, 1998, 2002, na 2010
Nyota wa zamani wa Liverpool na West Ham Rigobert Song amekimbizwa hospitalini akiwa katika hali mahututi baada ya kuugua kiharusi.
Song, 40, ambaye ni mjomba wa aliyekuwa mchezaji wa Arsenal, West Ham na Charlton Athletic Alex Song, alichezea timu ya taifa ya Cameroon mechi 137.
Taarifa zinasema alikuwa nyumbani kwake Odza, Yaounde alipopatwa na kiharusi na akakimbizwa hospitalini siku ya Jumapili.
Song, ambaye alikuwa nahodha wa Indomitable Lions, ndiye kocha mkuu wa timu ya taifa ya Chad, kazi aliyokabidhiwa mwishoni mwa mwaka jana.
Ndiye mchezaji aliyechezea timu ya taifa ya Cameroon mechi nyingi zaidi.
Wachezaji wengine nyota wa Cameroon, akiwemo Samuel Eto'oo, wamemtakia afueni ya haraka.
"Namtakia ndugu yangu mkubwa ujasiri na uponaji wa haraka," ameandika kwenye Twitter na Instagram.
Song
Image captionUjumbe wa Eto'o katika Instagram
Song alicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa dhidi ya Mexico mwaka 1993 na alikuwa nahodha wa Cameroon kwa miaka 10 tangu Eto'o alipochukua majukumu hayo 2009.
Alistaafu soka ya kimataifa 2010 baada ya kucheza Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment