TANGAZO


Wednesday, October 5, 2016

Raia wa Uganda Kazibwe kutowania wadhifa wa mwenyekiti AU

Bi Specioza Kazibwe

Image copyrightSPECIOZA KAZIBWE, FACEBOOK
Image captionBi Specioza Kazibwe
Makamu wa rais wa zamani wa Uganda Dkt Specioza Wandira Kazibwe, aliyekuwa mmoja wa waliopendekezwa kuwania wadhifa wa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU) amejitoa kwenye kinyang'anyiro hicho.
Juhudi za kutafuta mrithi wa Nkosazana Dlamini-Zuma zilianza upya Julai baada ya viongozi wan chi za Afrika kukosa kuafikiana kuhusu wagombea watatu waliokuwa wamewasilishwa.
Kando na Dkt Kazibwe, kulikuwa pia na waziri wa mambo ya nje wa Botswana Dkt Pelomoni Venson-Moitoi aliyeungwa mkono nan chi za Jumuiya ya Maendeleo ya kusini mwa Afrika (SADC) na waziri wa mambo ya nje wa Equatorial Guinea Agapito Mba Mokuy aliyeungwa mkono na nchi za Afrika ya kati.
Dkt Kazibwe, aliyehudumu kama makamu wa rais kati ya 1994 na 2003, alikuwa bado ana nafasi ya kuwania tena lakini kwa mujibu wa gazeti la serikali ya Uganda la New Vision, wanadiplomasia wakuu nchini humo wameamua kwamba hana nafasi nzuri ya kushinda.
Katibu katika wizara ya mambo ya nje ya Uganda James Mugume amenukuliwa na gazeti hilo akisema Uganda itaunga mkono wagombea wengine kutoka kanda ya mashariki mwa Afrika kutakapokuwa na msimamo mmoja.
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Kenya kuwania wadhfa wa mwenyekiti wa umoja wa Afrika AU
Image captionWaziri wa maswala ya kigeni nchini Kenya kuwania wadhfa wa mwenyekiti wa umoja wa Afrika AU
Siku chache zilizopita, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alitangaza kwamba waziri wa mambo ya nje wa Kenya Amina Mohamed atawania wadhifa huo.
Mwenyekiti mpya sasa amepangiwa kuchaguliwa Januari mwaka 2017 kwenye mkutano utakaofanyika makao makuu ya AU, Addis Ababa.

No comments:

Post a Comment