TANGAZO


Wednesday, October 5, 2016

Nigeria kuuza ndege za rais kupunguza ubadhirifu

Rais Buhari

Image copyrightAFP
Image captionRais Buhari, aliyeingia madarakani mwaka jana, aliahidi kukabili rushwa na ubadhirifu
Nigeria imetangaza kwamba itauza ndege mbili zinazotumiwa na rais wa nchi hiyo kama njia ya kupunguza matumizi mabaya ya pesa za umma.
Msemaji wa Rais Muhammadu Buhari, Garba Shehu, amesema ndege hizo mbili kati ya 10 zinazotumiwa na rais wa nchi hiyo zitauzwa kama sehemu ya kupunguza 'ubadhirifu' wa serikalini.
Serikali imeweka tangazo magazetini kwamba inauza ndege hizo, moja aina ya Falcon 7X na nyingine Hawker 4000.
Bw Shehu amesema Rais Buhari ndiye aliyeidhinisha matangazo hayo.
Ameongeza kwamba baadhi ya ndege nyingine za rais zitakabidhiwa jeshi la wanahewa la nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment