Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali (Mst) Salum Kijuu akimueleza Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya hatua zinazoendelea kuchukuliwa na serikali katika kurudisha hali baada ya tetemeko la ardhi kutokea mkoani huko.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali (Mst) Salum Kijuu wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Elimu na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akikagua vifaa ndani ya maabara katika shule ya sekondari ya Ihungo ambayo pia iliathiriwa kiasi kikubwa na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani kagera mapema mwezi September 2016.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akiongea na baadhi ya wafanyakazi waliopo katika eneo la ujenzi mpya wa shule ya sekondari ya Ihungo na kuwataka kufanya kazi kwa viwango stahiki na kwa wakati pamoja na wakijiepusha na vitendo vya wizi wa vifaa vya ujenzi.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akioneshwa baadhi ya majengo yatayojengwa upya katika shule ya sekondari ya Nyakato ambayo pia baadhi ya majengo yake yaliathiriwa na tetemeko la ardhi hiyo kuifanya kuamuliwa kujengwa upya.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akimuonesha jambo mwanafunzi mwenye ulemavu katika shule ya msingi Mgeza Mseto iliyopo mkoani kagera alipoitembelea kuona namna ilivyoathiriwa na tetemeko la ardhi kwenye baadhi ya majengo yake.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akiwaeleza jambo watoto wenye ulemavu wa ngozi (ALBINISM) wa shule ya Msingi ya Mgeza Mseto iliyopo mkoani kagera alipoitembelea kuona namna ilivyoathiriwa na tetemeko la ardhi kwenye baadhi ya majengo yake.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akiwaeleza jambo watoto wenye ulemavu wa ngozi (ALBINISM) wa shule ya Msingi ya Mgeza Mseto iliyopo mkoani kagera alipoitembelea kuona namna ilivyoathiriwa na tetemeko la ardhi kwenye baadhi ya majengo yake.
Na Benedict Liwenga-Maelezo
NAIBU Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi
Stella Manyanya leo amewasili Mkoani Kagera na kutembelea miundombinu ya sekta
ya elimu ili kujionea namna serikali inavyorejesha hali kama awali kutokana na
tetemeko la ardhi lililotokea September 10 mwaka huu.
Akiwa katika shule ya sekondari ya Ihungo, Mhandisi Manyanya
amewataka wakandarasi waliopewa dhamana ya kusimamia ujenzi upya wa majengo
mapya ya Shule za Ihungo na Nyakato kujenga kwa kuzingatia viwango sahihi
kulingana na maelekezo ya wataalam wa miamba.
“Mmepewa dhamana ya kusimamia ujenzi upya wa shule hii,
nawaombeni muzingatie viwango sahihi wakati mnajenga hasa kwa kuangalia
mapendekezo ya wataalam wa miamba waliyoyatoa ili kuyaweka majengo katika hali
ya usalama” Alisema Mhandishi Manyanya.
Aidha Mhandisi Manyanya amewatahadharisha wakandarasi wenye
tabia ya kudokoa vifaa vya ujenzi kutothubutu kufanya hivyo kwani yeyote
atayeiba vifaa hivyo atachukuliwa hatua za kisheria.
Katika kuhakikisha wanafunzi wenye ulemavu tofauti wanapata
elimu sawa Mhandisi Manyanya amewataka walimu wa shule ya msingi Mgeza Mseto
kutenda haki sawa wanafunzi wote bila kujali aina ya ulemavu alionao
mwanafunzi.
Katika hatua nyingine Mhandisi Manyanya amezitaka shule hasa
za sekondari nchini kuanzisha mashamba darasa yatakayowawezesha wanafunzi
kujifunza kwa vitendo shughuli za kilimo na kusaidia kuifanya shule kuwa na
hifadhi ya kutosha ya chakula.
Kwa upande wa walimu Mhandisi Manyanya amewapongeza walimu
wa wilaya ya Bukoba kwa kujituma na kuwekeza katika kilimo cha migomba na
kuwataka walimu kote nchini kuiga mfano huo ili kuwa na chakula cha kutosha na
kujiongezea kipato cha kuendesha maisha yao ya kila siku.
No comments:
Post a Comment