Meneja Mkuu wa Kampuni ya Fast jet, John Corse (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kampuni hiyo kuanza kutumia ndege mpya aina ya Embraer 190 kusafirisha abiria. Kulia ni Ofisa Uhusiano na Masoko wa kampuni hiyo, Lucy Mbogoro.
Ofisa Uhusiano na Masoko wa kampuni hiyo, Lucy Mbogoro (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Fast jet, John Corse (katikati), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo. Kushoto ni Ofisa Mkuu wa Huduma kwa Wateja, Christina Kausan.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Dotto Mwaibale
WANANCHI wametakiwa kuchangamkia usafiri wa ndege wa Kampuni ya Fast jet baada ya kampuni hiyo kuanza kutumia ndege mpya aina ya Embraer 190 ambayo ni nafuu zaidi kwa matumizi.
Mwito huo umetolewa na Dar es Salaam leo na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Fast jet, John Corse wakati akizungumza na waandishi wa habari jana kuwa ndege hizo ni rahisi kwa matumizi ya usafiri hapa nchini.
Alisema kuwa ndege hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 108 aliongeza kuwa zitahudumia kwa miezi 6 huku ikitoa nafasi kwa mafunzo wa marubani wa Fast jet hapa nchini.
Aliongeza kuwa kwa kuwa Fast jet hapa nchini imepata hasara kiuendeshaji hivyo ndege hizo kwa kuwa hazitumii matufa mengi itasaidia kuiimarisha biashara.
" Hii imetokea tu kuwa wakati serikali imeleta aina ya ndege zisizotumia mafuta mengi na sisi tulikuwa pia tumeshaanza mchakato huo na hivyo kwa sasa binafsi naona kuwa watanzania watanufaika zaidi" alisema Corse.
Pia aliipongeza serikali kwa kuleta ndege mpya aina ya Bombardier 8, Q400 ambazo zinaenda mikoa ya Rukwa, Mara, Kagera na Dodoma ambapo ndege za Fast jet hazifiki.
Alisema kwa kuwa lengo la Fast jet ni kuwapatia watanzania huduma nafuu za usafiri wa anga hivyo inafurahia pale ambapo inaona kuwa ndege za serikali zinafika mikoa ambayo Fast jet haifiki.
Alisema kuwa kwa kupeleka ndege kwenye mikoa hiyo ni hatua ambayo inatimiza lengo la Fast jet la kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora za anga kwa bei rahisi na kwa wakati.(Imeandaliwa na Dotto Mwaibale)
No comments:
Post a Comment