Zao aina ya Mirungi likiteketezwa kwa moto.
Mkulima wa zao la Mirungi Johnson Charles Kangara akiwa ameshika mafuta ya taa tayari kwa ajili ya kuteketeza shamba lake la Mirungi.
DC Staki akiwasisitiza wananchi kutojihusisha na kilimo cha zao la Mirungi.
Na Mathias Canal, Kilimanjaro
MWISHONI mwa mwezi Septemba mwaka huu Uongozi wa Wilaya ya Same ulitangaza vita dhidi ya wakulima wa Bangi, na Mirungi huku akitangaza kuwa kifungo cha miaka 30 kitawahusu wakulima wote wanaojishughulisha na kilimo hicho haramu kwani Bangi na Mirungi ni hatari kwa afya za watumiaji na kuisababishia serikali hasara kwa kutopokea Kodi.
Kiama hicho kilitangazwa na Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe Rosemary Staki Senyamule wakati akikabidhiwa mradi wa Ruvu muungano uliojumuisha zahanati sita, Nyumba mbili za waganga, matanki saba ya kuvuna maji na madarasa 54, ofisi 16 za walimu, vyumba na vyoo vya chuo cha ufundi makanya uliofadhiliwa na shirika la World Vision Tanzania.
DC Staki alisema kuwa kwa asilimia kubwa serikali imekuwa ikiwadhibu wanaoingiza Mirungi na Bangi sokoni huku ikiwasahau kuwachukulia hatua wale wote wanalima zao hilo.
Hivi karibu katika kijiji cha kisesa kata ya Vudee Wilayani humo ilibainika kuwa kuna wakulima wa Mirungi ambao wanajihusisha na zao hilo kwa muda mrefu pasina serikali kuwabaini na kuwa sugu kwa kilimo hicho hatimaye kukiona kama kilimo cha halali.
DC Staki alipotangaza kiama cha kukabiliana na wale wote wanaojihusisha na kilimo hicho aliahidi kuwatafuta wakulima hao na hatimaye kuwachukulia hatua za kisheria na kuhakikisha kuwa Wilaya ya same inakuwa safi pasina kuwa na Mirungi.
Hata hivyo katika ziara yake ya kazi Mhe Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki alipozuru kijiji cha kisesa kata ya Vudee alifanikiwa kumuweka chini ya ulinzi mkulima wa zao la Mirungi Johnson Charles Kangara na hatimaye kumuelekeza kuwasha kiberiti yeye mwenyewe katika shamba zima na kuchoma zao hilo.
DC Staki ameahidi kuhakikisha Wilaya ya Same inasifika kwa kilimo cha mazao mengine rafiki katika jamii ya Biashara na chakula na kuteketeza mazao yote haramu.

No comments:
Post a Comment