TANGAZO


Tuesday, October 11, 2016

Christian Benteke afunga bao la kasi zaidi mechi za Kombe la Dunia

Christian Benteke

Image copyrightREX FEATURES
Image captionBenteke amefungia Ubelgiji mabao manane
Mshambuliaji wa Ubelgiji Christian Benteke alifunga bao la kasi zaidi katika mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia, baada ya kufunga bao sekunde 8.1 dhidi ya Gibraltar.
Mchezaji huyo wa Crystal Palace alifunga mabao matatu wakati wa mechi hiyo ya Kundi H ambayo Ubelgiji walishinda 6-0. Wafungaji wengine walikuwa Eden Hazard, Axel Witsel na Dries Mertens.
Bao hilo la kwanza la Benteke pia ndilo la kasi zaidi kuwahi kufungwa na mchezaji wa Ubelgiji.
Benteke alivunja rekodi ya awali ya bao la kasi zaidi mechi za kufuzu Kombe la Dunia iliyokuwa ya sekunde 8.3, ambayo iliwekwa na Davide Gualtieri wa San Marino dhidi ya England mwaka 1993.
Katika mechi nyingine, kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba alifungia Ufaransa bao la pekee ushindi wao wa 1-0 dhidi ya Uholanzi.
Sweden, walilaza Bulgaria 3-0, Ureno nao wakashinda Visiwa vya Faroe 6-0.

No comments:

Post a Comment