TANGAZO


Sunday, October 2, 2016

ACT YAZINDUA HARAMBEE YA UJENZI WA KANISA JIJINI DAR

KANISA la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) linaloendesha shughuli zake katika ukumbi wa Utoji, Sinza Mapambano jijini Dar limezindua harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo rasmi.

Akizungumza katika misa iliyofanyika eneo hilo, mchungaji wa kanisa hilo Pastor Sos Mabele alisema kuwa harambee hiyo imezinduliwa kanisani hapo kwa waumini na watu mbalimbali kuweka ahadi au kuchangia moja kwa moja fedha kwa ajili ya ujenzi wa kanisa unaotarajiwa kuanza mwisho wa mwaka huu. 

Mbali na hayo Mchungaji huyo aliwataka watu mbalimbali wajitokeze kuchangia  ujenzi wa kanisa hilo bila kujali madhehebu au dini, kwa kuwa Mungu ni wa wote  ambapo pia alisema kuwa zoezi la harambee  litaisha tarehe 25 mwezi huu kwa walioahidi wote kutimiza ahadi zao.

“Sisi kanisa letu kama linavyosema kuwa ni All- Nations Christian Tabernacle yaani hekalu la makanisa ya mataifa yote, hivyo hatubagui mtu kwa dhehebu wala dini na wote wanakaribishwa kila jumapili kwenye ibada zetu,” alisema Pastor Sos na kuwataka watu waendelee kuwasiliana naye kwa ahadi na michango kupitia namba 0784935855.

Naye mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Kanisa hilo, bwana Ibrahimu Chanikicha, aliwashukuru wote wanaoendelea kuchangia kwa hali na mali na kuwaomba waendelee kuwa na moyo huohuyo.

Mchungaji wa Kanisa la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) Sos Mabele akisali wakati akifungua Ibada hiyo iliyokuwa ni ya ufunguzi wa Harambee ya uchangiaji wa ujenzi wa Kanisa.
Mmoja ya waumini akisoma neno la Mungu wakati Mchungaji akiwaongoza.
Waumini wakimsikiliza kwa makini Baba Mchungaji akifundisha neno.
Katibu wa kamati ya ujenzi Debora Simon (kulia) pamoja na waumini mwengine wakifuatilia neno.
Mchungaji wa Kanisa la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) Sos Mabele akiendelea kutoa mahubiri wakati wa Ibada hiyo ya uzinduzi wa Harambee ya uchangiaji kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa. 
Mweka Hazina wa Kanisa hilo Bwana Geofrey Raymond akifuatilia Ibada kwa makini.
Waumini wakiendelea kufuatilia Ibada kwa makini.
Mmoja wa watoto akisoma Neno la Mungu wakati wa Ibada hiyo ya Uchangiaji kwa ajili ya Ujenzi wa Kanisa.
Wakijiandaa Kumtukuza Mungu.
Baadhi ya watoto wakiwa Ibadani.
Mchungaji wa Kanisa la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) Sos Mabele akiimba nyimbo za Sifa.
Mweka Hazina wa Kanisa hilo Bwana Geofrey Raymond akizungumza neno wakati wa Ibada hiyo.
Ibrahim Chanikicha Mwenyekiti wa kamati ya Ujenzi akizungumza jambo.  
Waimbaji wakiendelea kumtukuza Mungu  kwa njia ya Nyimbo za Sifa.
Waumini wakiimba nyimbo za Sifa.
Muda wa Maombezi ulifika ambapo Mchungaji wa Kanisa la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) Sos Mabele aliwaombea watumishi mbalimbali.
Wakiendelea kusifu na Kuabudu.(Picha zote na Fredy Njeje)

No comments:

Post a Comment