Baadhi ya madawati yaliyokabidhiwa jana na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa bungeni mwanzoni mwa mwaka huu na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe ya kutengeneza madawati 20,000.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa
wamekaa kwenye madawati mara baada ya makabidhiano yaliyofanyika Mkoani Mwanzan
jana na Naibu Waziri wa Wizara ya
Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani kwa
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , John Mongela
ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa bungeni mwanzoni mwa mwaka huu
na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe.
WIZARA ya Maliasili na Utalii kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imekabidhi
madawati 12,115 mkoani Mwanza ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa bungeni
mwanzoni mwa mwaka huu na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe
ya kutengeneza madawati 20,000.
Makabidhiano
hayo baina ya TFS na Serikali yalifanyika kitaifa kwenye Uwanja wa chuo cha
Mafunzo ya Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi.
Naibu wa Waziri wa Wizara
hiyo , Ramo Makani alitoa mwezi mmoja kwa uongozi wa TFS kuhakikisha unakamilisha
kutengenenza madawati 7,885 yaliyosalia kabla ya novemba mwezi huu
‘’ Pamoja na kufikia asilimia
61 ya lengo, nawaomba TFS muhakikishe idadi iliyobaki ya madawati inakamilika
ifikapo mwishoni mwa mwezi ujao’’ Alisema Makani.
Akizungumza kabla ya
kukabidhi madawati hayo, Mtendaji Mkuu wa TFS, Prof. Dos Santos Silayo bila
kutaja gharama iliyotumika alisema ofisi yake imechelewa kufikia asilimia 100
ya kutengeneza madawati 20,000 kutokana na kuwa na changamoto ya ucheleweshwaji
wa taratibu za uvunaji mbao katika baadhi
ya misitu.
TFS tumetekeleza agizo hili
kwa kulenga ngazi za chini kabisa za mfumo wa utendaji wa Wakala ambao ni wilaya. Hivyo katika kugawa idadi ya
utengenezaji madawati wa kanda ilizingatia idadi ya wilaya kwa kila kanda’’
alisema Prof. Silayo.
Waziri Makani alisema
madawati hayo yatagawiwa katika mikoa ya Simiyu., Kagera, Mara,Geita na Mwanza
ambayo itapokea madwati 2,580 yaliyokwisha tengenezwa.
Akizungumz kwa niaba ya Wakuu
wa Mikoa ya Tanzania Bara, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela aliwapongeza
TFS na kuahidi kuyatunza madwati hayo ili yatumike kwa muda mrefu kwa manufaa
ya wanafunzi.
No comments:
Post a Comment