Mkuu
wa Wilaya ya Bukoba Bw. Deodatus Kinawiro akikagua ujenzi wa miundombinu
iliyoharibiwa na tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Mkuu
wa Wilaya ya Bukoba Bw. Deodatus Kinawiro akiongea na Baraza la Madiwani la
Halmashauri ya Bukoba na kuwataka kuacha kulalamika hasa katika kipindi hichi
cha kurudisha hali ya kawaida baada ya tetemeko la ardhi kutokea bali watafute
njia itakayoleta majawabu ya mambo yanayojitokeza.
Baadhi
ya Madiwani wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Bw. Deodatus Kinawiro wakati
wa kikao cha dharura cha baraza hilo.
Mkuu
wa Wilaya ya Bukoba Bw. Deodatus Kinawiro akiongea na wanafunzi wa shule ya
msingi Kashai iliyoripotiwa na moja ya kituo cha televisheni nchini kuwa shule
hiyo imefungwa kutokana na athari za tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
5Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Bw. Deodatus Kinawiro akiongea na
walimu wa shule ya msingi Kashai alipowatembelea ili kuona maendeleo ya
wanafunzi baada ya taarifa za upotoshaji zilizotolewa na moja ya kituo cha
televisheni nchini kuwa shule hiyo imefungwa kutokana na athari za tetemeko la
ardhi mkoani Kagera.
Mkuu
wa Wilaya ya Bukoba Bw. Deodatus Kinawiro akikagua nyumba za muda za walimu wa Shule ya Msingi Kaishaza mkoani Kagera baada ya nyumba zao kuathirika na tetemeko
la ardhi mkoani Kagera.
No comments:
Post a Comment