TANGAZO


Friday, July 1, 2016

RAIS WA RWANDA PAUL KAGAME AWASILI NCHINI TANZANIA KWA ZIARA YA SIKU MBILI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (kulia) akiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame, wakati walipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Waziri mwenzake wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Louise Mushikiwabo kabla ya kusaini Muhtasari wa Tume ya Ushirikiano wa Pamoja kati ya Tanzania na Rwanda. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (kulia) akiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame,wakishuhudia Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Louise Mushikiwabo (kushoto) wakisaini Muhtasari wa Tume ya Ushirikiano wa Pamoja kati ya Tanzania na Rwanda. 
Rais wa Rwanda Paul Kagame akizungumza kwenye ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kuwasili nchini Tanzania kwa ziara ya siku mbili.Nyuma yake aliyekaa ni mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (kulia) akimpongeza mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumzia ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda huku akisikilizwa na baadhi ya viongozi wa Tanzania na Rwanda. Aliyekaa nyuma yake ni mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame wakati Kushoto mbele ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan(aliyevaa mtandao mweupe) na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumzia ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda huku akisikilizwa na baadhi ya viongozi wa Tanzania na Rwanda. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (kulia) akimuongoza mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame kutoka nje ya ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kuzungumza na wananchi juu ya ziara ya Rais Kagame. (Picha zote na Hussein Makame-MAELEZO)

No comments:

Post a Comment