TANGAZO


Thursday, July 7, 2016

RAIS MAGUFULI AWATAKA WAISLAMU KUDUMISHA AMANI NCHINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya kuhuduria Baraza la Eidd liliofanyika Kitaifa jana Jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia  wakati wa Baraza la Eidd  katika viwanja vya Karimjee jana Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaji Ally Hassan Mwinyi na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum. 
Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Alhaji Musa Zubery akitoa salaam za waislamu kwa mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jphn Pombe Magufuli ( wa kwanza kushoto) wakati wa Baraza la Eidd  leo Jijini Dar es Salaam. Wa pili kutoka kushoto ni Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Mhe. Alhaji Ally Hassan Mwinyi na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akitete jambo na Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abubakar  Zubery( kushoto)  wakati wa Baraza la Eidd lilofanyika kitaifa katika viwanja vya Karimjee jana Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda. 
Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Mhe. Alhaji Ally Hassan Mwinyi akiwa katika viwanja vya Karimjee alipohudhuria Baraza la Eidd jana Jijini Dar es Salaam 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa na akifurahia jambo na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum, katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa mara baada ya  ya kumalizika kwa Baraza la Eid jana Jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu nchini mara baada ya kumalizika kwa Baraza la Eidd lililofanyika katika viwanja vya Karimjee jana Jijini Dar es Salaam. 
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR –TAMISEMI) Mhe. Suleiman Jaffo akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda. Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mhe. Abdallah Ulega. 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa na akifurahia jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda wakati wa hafla ya Baraza la Eidd jana Jijini Dar es Slaam. 
Mku wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akifurahia jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kindondoni, Ally Hapi na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum wakati wa hafla ya Baraza la Eidd jana Jijini Dar es Salaam. 
Kikundi cha Kaswida cha Amani kikitumbuiza wakati wa hafla ya Baraza la Eidd jana Jijini Dar es Salaam. 
Waumini wa dini ya Kiislamu wakifuatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (hayupo pichani) wakati wa hafla ya Baraza la Eidd jana Jijini Dar es Salaam. 
Waumini wa dini ya Kiislamu wakifuatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (hayupo pichani) wakati wa hafla ya Baraza la Eidd jana Jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwaaga waumini wa dini ya Kiislamu mara baada ya kumalizika kwa Braza la Eidd lilofanyika kitaifa katika viwanja vya Karimjee jana Jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Frank Shija, MAELEZO)

Jonas Kamaleki, MAELEZO
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewaasa Waislamu nchini kudumisha amani, kuzuia vitendo vya rushwa na ufisadi ili kumpendeza Mwenyezi Mungu na kuendeleza matendo mema ili kuondoa changamoto zinazolikabili Taifa letu.

Rais ameyasema hayo jana alipokuwa akihutubia Baraza la Idd lililofanyika kitaifa jijini Dar es Salaam.

“Siku kuu hizi zinatuwezesha kutafakari juu ya mstakhabali wa Taifa letu ili kuleta amani ambayo si kwa waislamu tu bali kwa wananchi wote kwa ujumla,”alisema Rais Magufuli.

Ameongeza kuwa serikali anayoingoza itafanya kila liwezekanalo kuitunza amani ya Tanzania na kuendelea kuifanya nchi hii kuwa kisiwa cha amani.

Aidha, Rais Magufuli amewashukuru waislamu kwa mchango wao mkubwa katika maendeleo ya jamii ikiwemo suala la elimu, maji, afya ambavyo vimewanufaisha watanzania hasa wenye maisha ya chini.

“Kwa upande wetu serikali itaendelea kuwaunga mkono katika juhudi zenu za kimaendeleo na ikibidi kutoa msaada pale unapohitajika,”alisema Magufuli.

Rais Magufuli pia ameahidi kulinda mali za waislamu zisichukuliwe na watu wasiohusika ikiwemo kuweka mikataba ya kitapeli. Amekemea tabia ya wawekezaji ambao wanatoa ahadi za uwekezaji katika mali za waislamu lakini hawatimizi ahadi zao.

Amesema kuwa serikali haitaruhusu wajanja wachache kudhurumu mali za waislamu na kuongeza kuwa serikali itashirikiana na BAKWATA kulinda mali hizo.

Akionyesha furaha yake kwa kijana aliyesoma Koran, Samiu Musa, Rais Magufuli ameamua kumpatia Tsh. milioni 2 kwa ajili ya kumsaidia katika safari yake ya kwenda Urusi. Rais pia amekizawadia kikundi cha uimbaji cha Amani Tsh. milioni 2 kwa kuimba vizuri.

Rais Magufuli amesema kuwa miezi takribani minane ya serikali ya awamu ya Tano, elimu bure imeanza kutolewa, vitendo vya rushwa na ufisadi vimeanza kudhibitiwa na ukusanyaji wa kodi umeongezeka. 

Serikali imejipanga kutumia raslimali zilizopo nchini kuwanufaisha wananchi na kuwafanya waishi maisha mazuri licha ya kwamba wapo wachache watakaoguswa na hatua hizo, alisema Rais Magufuli.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Baraza la Waislam Tanzania (BAKWATA), Alhaji Suleiman Lulila amesema BAKWATA imejenga Chuo Kikuu Dodoma ambacho kitafunguliwa mapema mwakani ili kusaidia katika kuendeleza utoaji wa elimu bora nchini.

Ameongeza kuwa BAKWATA itaendelea kushirikiana na serikali katika shughuli za kimaendeleo na kulinda amani nchini na kulinda umoja na mshikamano kwa watanzania.


Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kushiriki Baraza la IDD akiwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment