TANGAZO


Friday, June 10, 2016

MATUKIO MBALIMBALI MITAANI LEO JIJINI DAR ES SALAAM

Takataka zilizorundikana katika machinjio ya kuku katika Soko la Kisutu ambazo huchelewa kuzolewa na kupelekea kutoa harufu mbaya na wadudu ambao imekuwa kero kwa wafanyabiashara na watumiaji wa Machinjio hayo. 
Chemba inayotiririsha maji taka katika Mtaa wa Kitumbini jijini Dar es Salaam imekuwa kero ya muda mrefu kwa watumiaji wa barabara hiyo na wafanyabiashara katika eneo hilo. 
Mama ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akiwa na mtoto wake pembezoni mwa barabara ya Ohio akiwa ana omba msaada kwa wapiti njia mapema hii leo jijini Dar es Salaam. 
Dereva wa basi la mwendo kasi  akitii sheria za usalama barabarani kwa kusubiri watembea kwa miguu kuvuka katika alama za punda milia katika kituo cha Posta ya Zamani mapema hii leo jijini Dar es Salaam.  
Dereva wa daladala linalofanya safari zake kati ya Makumbusho na Posta akipakia abiria mahali ambapo hapana kituo na hivyo kuhatarisha usalama wa abiria na watumiaji wengine wa barabara hiyo kama alivyokutwa na mpiga picha katika makutano ya barabara ya azikiwe na Jamhuri mapema hii leo jijini Dar es Salaam. 
Mtu ambaye jina lake halikuweza kupatikana haraka mwenye ulemavu wa mguu akiwa amelala chini baada ya kutolewa nje ya ofisi za Shirika la Bima la Taifa na walinzi wa shirika hilo mara baada ya kutaka kuomba msaada wa fedha za matibabu kwa Mkurugenzi wa shirika hilo. (Picha zote na Eliphace Marwa) 

No comments:

Post a Comment