Na Daudi Manongi-MAELEZO
MKUU wa Mkoa wa Dar
es Salaam Mhe.Paul Makonda atazindua maonyesho ya kwanza ya simu halisi (original)
katika viwanja vya Posta jumamosi ya Tarehe 11 mwezi huu kuanzia saa 3 asubuhi
mpaka saa 12 jioni.
Lengo kuu la
kufanyika kwa maonyesho hayo ni kuwapa elimu wateja wa simu kujua ipi ni simu
fake na ipi ni original kutoka kwa
makampuni hayo ya simu,pia kwa kushirikiana na TCRA watatoa elimu kuhusu
matumizi sahihi ya simu na mitandao ya kijamii.
Lengo la tatu ni
kuhakikisha wateja wanajipatia simu original kwa bei nafuu kabla ya simu fake
kuzimwa tarehe 16 mwezi huu.
Nae Kaimu Katibu
mtendaji wa Baraza la watumiaji wa huduma za mawasiliano(TCRA-CCC),Mary Msuya
amewashauri watumiaji wa simu nchini kununua simu katika maduka ya simu na
kuomba risiti ya dhamana ya muda wa matumizi ya bidhaa usiopungua miezi 12.
Aidha aliwataka
wafanyabishara wasio waaminifu kuacha mara moja kuingiza bidhaa feki nchini kwa
njia za panya kwani serikali iko makini katika kusimamia suala hilo.
Kwa upande wake
mwakilishi wa makampuni ya simu Meneja mauzo wa kampuni ya Tecno Bw.Fred
Kadilana ametoa wito kwa watumiaji wa simu kuja kwa wingi ili kujipatia simu
zenye ubora wa hali ya juu kutoka kampuni mbalimbali.
Wateja wa simu za
mkononi watajipatia simu original kutoka katika maonyesho hayo kwa bei nafuu
kutoka kwa makampuni ya simu ya Samsung,Tecno,Startimes,Huawei na Itel uku
kukiwa na ushiriki wa makampuni ya simu ya Vodacom,Tigo na TTCL.
Katika maonyesho hayo
Taasisi mbalimbali za serikali zitashiriki kama mamlaka ya mawasiliano Tanzania
(TCRA), Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano (TCRA-CCC) na Mfuko
wa mawasiliano kwa wote (UCSAF).


No comments:
Post a Comment