Jaji wa Mahakama ya rufani Bw. Shaban Lila akisaini hati ya kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya uapisho ya Jaji Kiongozi na Jaji wa Mahakama ya rufani leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Kiongozi Bw. Ferdinand Wambali (kulia) na Jaji wa Mahakama ya rufani Bw. Shaban Lila baada ya kuwapisha leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya Pamoja na baadhi ya viongozi wakati wa uapisho kutoka kulia ni Jaji Mkuu Mh. Chande Othuman, Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa, Jaji Kiongozi Mh. Ferdinand Wambali, Jaji wa Mahakama ya rufani Mh. Shaban Lila na Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya wageni waliohudhuria hafla ya uapisho ya Jaji Kiongozi na Jaji wa Mahakama ya rufani leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria hafla ya uapisho ya Jaji Kiongozi na Jaji wa Mahakama ya rufani leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Bw. Hussein Kattanga akimueleza jambo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa wakati wa hafla ya uapisho ya Jaji Kiongozi na Jaji wa Mahakama ya rufani leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Bw. Hussein Kattanga, Kutoka kulia ni Jaji Mkuu Mh. Chande Othmani, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John William Kijazi.
Hussein
Makame-MAELEZO
MAHAKAMA ya Tanzania
imepiga hatua kubwa kwa miaka mitatu iliyopita katika kusikiliza na kuamua mashauri
yaliyowasilishwa kwenye ngazi mbalimbali za mahakama nchini.
Hayo yamesemwa wakati
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipowaapisha
Jaji Shabani Ally Lila kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani na Jaji Ferdinand
Wambali kuwa Jaji Kiongozi, Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Akizungumza baada ya
uapisho huo Jaji Kiongozi, Wambali alibainisha mafanikio hayo ya mahakama na
kuahidi kuongeza kasi ya kutekeleza majukumu ya kusikiliza na kuamua mashauri
yanaypowasilishwa mahakamani.
Alisema moja ya kazi
kubwa ya mahakama ni kusikiliza mashauri na kuyatolea maamuzi kwa mujibu wa
sheria na taratibu zilizowekwa.
“Hakuna shaka kwamba
zipo changamoto nyingi kuhusiana na uendeshaji wa mashauri lakini pia
tumepiga hatua kubwa kwa miaka mitatu iliyopita katika usikilizaji wa
mashauri” alisema Jaji Wambali na kuongeza:
“Kwa hiyo kasi ambayo
imekuwa ipo mimi naahidi kufanya kazi kwa bidii na nguvu zote kwa jinsi
Mwenyezi Mungu anavyonijalia kuhakikisha kwamba tunaendeleza pale ambapo
wenzangu wamafikia”.
Jaji Wambali
alifafanua kuwa mahakama inayo timu nzuri ya majaji na anaamini atashirikiana
kwa dhati na watumishi wengine kuhakikisha kwamba anatatua matatizo ya
wananchi.
“Lakini kama
mnavyofahamu mahakama iko kwenye maboresho mengi na hasa kuhakikisha mahakama
inakuwa karibu na wananchi na mimi nitalisimamia hilo kwamba mahakama isiwe
chombo kinachoogopwa na wananchi bali kiwe chombo ambacho kinafikiwa na
wananchi kwa karibu” alieleza Jaji Wambali.
Alisema mambo manne
ya msingi aliyoyaapa ndiyo yatakamuongoza kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na
taratibu bila woga, upendeleo, chuki wala huba.
“Hayo ndio mambo
makubwa manne ambayo jaji yeyote yanamuongoza katika kutoa haki kwa hiyo hilo
ndilo linaloahidi kulitekeleza kwa nguvu zangu zote” alisema.
Akizungumzia kesi
kukaa muda mrefu bila kuamuliza, Jaji Wambali alisema sheria inataka kesi ya
madai isikae zaidi ya miaka miwili na mahakama imejipangia muda wa miezi 18 wa
kusikiliza kesi hizo, hata hivyo ameomba ushirikiano kwa wadau ili kufanikisha
lengo hilo.
“Ndio maana nimesema
ni lazima tushirikiano na wadau wote kwani wakati mwingine kesi zinaahirishwa
kwa sababu ya wadau. Lakini katika miaka hii miwili iliyopita sasa wananchi
wanatambua kwamba kesi zinaamuliwa kwa wingi sana kwa sababu kila Jaji, hakimu
amepangiwa kesi za kusikiliza kwa mwaka” alisema Jaji Wambali.
Alisema vipo vituo
ambavyo mahakimu na majaji wanamaliza kesi na wanatakiwa kwenda kwenye vituo
vingine kusaidia, hivyo watajitahidi kwa nguvu zote kuhakikisha kwamba wanalitekeleza
hilo kwa nguvu zote.
Kwa upande wake, Jaji
wa Mahakama ya Rufani, Jaji Shabani Ally
Lila, alisema kuwa anakwenda Mahakama ya Rufani kuongeza nguvu kwenye
kusikiliza na kuamua mashauri.
“Najua Mahakama ya Rufani
inashughulika na kusikiliza na kuamua mashauri, kwa hiyo tutashirikiana na
wenzangu kuona namna ambavyo tutakabiliana na mashauri ambayo sasa hivi yana
muda mrefu mahakamani”
alisema Jaji Lila.







No comments:
Post a Comment