Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kiwanga
Na Tiganya Vincent_MAELEZO-Dodoma.
JUMLA watuhumiwa wa dawa za kulevya 719 walikamatwa na kilo 141.27 za aina mbalimbali za dawa za kulevya za viwandani katika kipindi cha kuanzia Julai mwaka jana hadi mwezi wa tatu mwaka huu.
Takwimu hizo zimetolewa leo mjini Dodoma na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kiwanga wakati akisoma hotuba ya Wizara yake ya makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka ujao wa fedha.
Alisema kuwa kati ya watuhumiwa hao wanaume walikuwa 644 na wanawalikuwa ni 75.
Waziri huyo atizitaja dawa za viwandani zilizokamatwa na Jeshi la Polisi kuwa ni Heroin , cocaine, cannabis resin, morphine na mandrax.
Aidha , Mhe. Kitwanga alisema kuwa Jeshi la Polisi katika kipindi hicho lilifanikiwa kukamata kilo elfu 18,513 na gramu 415 za bhangi na kilo elfu 15,402 za mirungi zilikamatwa.
Alitaja idadi ya watuhimiwa waliokamatwa na dawa hizo zisizo ya viwandani kuwa wanawake ni 9,935 na wanawake 1,020.
Mhe. Kitwanga alisema kuwa Jeshi la Polisi katika mwaka ujao wa fedha litaongeza mapambano dhidi ya biashara ya dawa za kulevya na mtandao wa uingizaji na usambazaji wa dawa za kulevya nchini.
Waziri huyo aliliomba Bunge lipitishe jumla ya shilingi 864,106,290,105/= ili Wizara yake iweze kutekeleza majukumu yake katika mwaka ujao wa fedha.
Alisema kuwa kati ya fedha hizo shilingi 316,126,377,000/= ni za matumizi mengineyo, shilingi 500,056,492,000/= ni kwa ajili ya mishahara na shilingi 47,923,421,105 ni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya mandeleo.


No comments:
Post a Comment