Waziri Mkuu mpya wa New Zealand John Key ametupwa nje ya bunge na spika baada ya kukaidi kufuata kanuni za bunge.
Bunge hilo limekua na mjadala mkali kuhusu sakata ya akaunti za siri ambazo zinadaiwa kuwepo kisiwa cha Panama.
Spika wa Bunge David Carter ametetea hatua yake na kusema Waziri Mkuu alikaidi onyo la kutoheshimu kanuni za bunge, na hivyo hakua na kinga ila kumuadhibu, kama wabunge wengine.
Rekodi za bunge zimenakili kwamba Waziri Mkuu huyo aliwahi kutupwa nje ya bunge mara tatu wakati akiwa mbunge.
Hata hivyo si mara ya kwanza Waziri MKuu NewZealand anatupwa nje ya bunge.
Waziri Mkuu wa zamani Helen Clark alitupwa nje mwaka 2005 huku naye mtangulizi wake, David Lange akijipata pabaya miaka ya 1986 na 1987.
No comments:
Post a Comment