TANGAZO


Wednesday, May 11, 2016

Wafuasi wa Katumbi watimuliwa na polisi


Image copyright
Image captionMgombea urais DRC Moise Katumbi
Polisi kusini mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasi ya Congo wamewatawanya maelfu ya wafuasi wa mwanaisiasa, Moise Katumbi, anayehojiwa dhidi ya tuhuma za serikali kwamba ameajiri mamluki kutoka mataifa ya nje.
Wafuasi wa Katumbi waliingia mahakamani kwa lazima mjini Lubumbashi anakotarajiwa kufika kusikizwa kwa mara ya pili kesi dhii yake.
Wafuasi wake wanasema tuhuma hizo zimenuiliwa kutatiza kampeni yake ya kisiasa kumrithi rais Joseph Kabila.
Moise Katumbi amethibitisha rasmi siku chache zilizopita kwamba atogemba urais wa nchi hiyo katika uchaguzi utakao fanyika Novemba mwaka huu.

Image captionWafuasi wa Moise katumbi DRC
Mawakili wa Moise Katumbi wamesema Gavana huyo wa zamani wa jimbo lililo na utajiri wa madini - Katanga, alikabidhiwa barua ya kufika mahakamani mwishoni mwa juma.
Nyumba yake ilisakwa na walinzi wa serikali siku ya Jumamosi.
Katumbi amekana mashtaka na ameishutumu serikali kwa kutumia njia za kumchafulia jina.
Ubalozi wa Marekani mjini Kinshasa pia umetilia shaka tuhuma hizo.
Rais Joseph Kabila ambaye yupo madarakani tangu mwaka 2001 bado hajabainisha iwapo atajiuzulu mwaka huu kama inavyo takiwa kwenye katiba ya nchi.

No comments:

Post a Comment