TANGAZO


Wednesday, May 11, 2016

Tsvangirai: Fedha mpya sio suluhu kiuchumi


Image copyrightAFP
Image captionMorgan Tsvangirai

Chama cha upinzani nchini Zimbabwe kikiongozwa na Morgan Tsvangirai kinasema kuanzishwa kwa Bond Noti yaani Fedha ya Dhamana siyo suluhisho la tatizo la uchumi linaloikumba nchi hiyo na kesho watafanya kikao ili kutafuta la kufanya.
Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wa Tsvangirai, Luke Tamborinyoka amesema tatizo la uchumi ni matokeo ya sintofahamu iliyoanzia kwenye uchaguzi uliovurugwa mwaka 2013.
"Bahati mbaya kwa Zanu PF kuchapisha noti mpya haiwezi kuwa dawa kwa tatizo la kisiasa linalohitaji suluhu ya kisiasa.
Hizo Bond notes ni ushahidi wa ukatili wa serikali inayong'ang'ania kuongoza nchi" anasema Tamborinyoka. Gavana wa Benki kuu ya Zimbabwe RBZ John Mangudya alitangaza wiki iliyopita kuwa Zimbabwe itaanzisha noti mpya za fedha ya dhamana ili kuziba pengo la fedha linaloikumba Zimbabwe.
Fedha hizo zitadhaminiwa kwa dola milioni 200 kutoka Afrexibank iliyoko Misri.
Tangazo la Benki Kuu ya Zimbabwe la kuanzisha noti hizo mpya pamoja na kuwa na thamani ya dola ya Marekani na kutumika sambamba na dola hazitaweza kununua chochote nje ya nchi hali iliyoleta hofu kwa wakaazi wa nchi hii na kuanza kuondoa fedha zao kwenye Benki kote nchini.
Benki nazo zimeweka kiwango kidogo cha kuchukua kwa siku na wakati mwingine wateja huondoka mikono mitupu.

No comments:

Post a Comment