TANGAZO


Monday, May 9, 2016

WAWEKEZAJI SEKTA BINAFSI WAHIMIZWA KUWEKEZA KATIKA BIASHARA YA MATUNDA MKOANI TANGA

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage

Na Benedict Liwenga-MAELEZO, Dodoma.
WAWEKEZAJI kutoka Sekta Binafsi nchini wenye nia ya kufungua Viwanda vya juisi mkoani Tanga ikiwemo Wilaya ya Muheza wamehimizwa kuwekeza katika biashara hiyo mkoani humo.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage wakati wa kipindi cha maswali na majibu, ambapo Mhe. Mwijage alikuwa kijibu swali lililoulizwa na Mheshimiwa Balozi Adadi Mohamed Rajabu, Mbunge wa Muheza lililotaka kujua ni lini Serikali itajenga kiwanda cha matunda wilayani hapo na kuwaondolea usumbufu wakulima katika utafutaji masoko.

Mhe. Mwijage amesema kuwa tafsiri ya Serikali katika kujenga viwanda ni kwa serikali kuweka mazingira sahihi na wezeshi ili kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje wa sekta binafsi kujenga viwanda.

Aidha, aktika kutekeleza hilo Mhe. Mwijage ameeleza kuwa Sera na Mikakati mbalimbali shirikishi inatoa fursa kwa Sekta na Taasisi za uwekezaji kujenga viwanda na kunufaika na vivutio mbalimbali.

“Mkoa wa Tanga ikiwemo Wilaya ya Muheza wamejaaliwa kuwa na utajiri wa matunda aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na machungwa, maembe, machenza, mafenesi na mananasi, kwa kutambua upatikanaji wa matunda hayo, Wizara yangu inahimiza na kuhamasisha wawekezaji kutoka Sekta Binafsi wenye nia ya kufungua viwanda vya juisi mkoani Tanga wafanye hivo’’, alisema Mhe. Mwijage.

Amefafanua kuwa, mpaka sasa Kampuni ya M/s Sasumua Holding imeanzisha mradi mkubwa wa kulima matunda katika utaratibu utakaoshirikisho wananchi na kufikia mwezi Novemba, 2018 kiwanda cha juisi kitakuwa tayari kinafanya kazi.

“Mradi huu uko kwamsisi, Handeni mkoani Tangam hivyo ni tegemo langu kuwa mafaniko ya Mwekezaji huyo yatawavutia wawekezaji wengine”, alisema Mhe. Mwijage.

Ameongeza kuwa, Wizara kupitia Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) ina utaratibu wa kutoa ushauri jinsi ya kuanzisha mitaa ya viwanda kila mkoa ikiwa ni jitihada za kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi kuendeleza uzalishaji katika mikoa husika.

No comments:

Post a Comment