Ofisa Sheria wa Tume ya Kurekebisha Sheria Bw. Fredy Kandonga akifafanua kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu tafiti za kisheria zinazotarajiwa kufanyiwa kazi kwa kipindi cha Mwaka 2016/2017 ikiwemo Mapitio ya Sheria za Uwekezaji. Katikati ni Ofisa Sheria kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Bw. Hemed Lusungu na kulia ni Ofisa Habari wa Tume hiyo, Bw. Munir Shemweta.
Frank
Mvungi-Maelezo.
SERIKALIkatika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/2017 inatarajia kufanya mapitio katika
sheria mbalimbali ili kutoa mapendekezo yatakayowezesha kufanyika kwa marekebisho
au kutungwa kwa sheria mpya kulingana na
mahitaji ya sasa.
Kauli hiyo
imetolewa leo jijini Dar es salaam na afisa Sheria wa Tume ya Kurekebisha
Sheria Tanzania Bw. Hemed Lusungu wakati
wa Mkutano na vyombo vya Habari uliolenga kutoa mwelekeo wa utekelezaji wa
majukumu ya tume hiyo.
Akifafanua Lusungu amesema kuwa Sheria zitakazofanyiwa
utafiti ili ziboreshwe na kuendana na Kasi ya Serikali ya awamu ya Tano ni
sheria za uwekezaji (Review of the legal
frame work Governing Investiment for viable economic growth).
“Tunataka
sheria katika eneo la Uwekezaji ziendane na dhana ya mheshimiwa Rais John Pombe
Magufuli inayolenga kukuza viwanda vya ndani hivyo ni lazima tutazame eneo hili
ili kuwa na sheria zitakayowezesha suala hili” alisisitiza Lusungu.
Akizungumzia
mapitio katika sheria za Usafirishaji Lusungu amesema kuwa lengo ni kuhakikisha
kuwa kunakuwa na sheria zinazokidhi mahitaji ya sasa hivyo utafiti wao utatoa
mapendekezo ili kulinda haki za wasafiri na wasafirishaji.
Alisema faida
za Tafiti zinazofanywa na Tume hiyo ni kusaidia kwa kiasi kikubwa kuchochea
marekebisho ya sheria mbalimbali na pia kusaidia kutungwa kwa sheria mpya
kulingana na mahitaji ya wakati akitolea mafano sheria ya Ununuzi wa Umma sura
ya 410.
Aliongeza
kuwa sheria hiyo imekuwa ikilalamikiwa kurefusha mchakato wa manunuzi na
kufanya bei ya bidhaa au huduma kuwa kubwa.
Kwa
kuzingatia umuhimu wa Sheria hiyo Tume imeshafanya mapitio katika maeneo husika
na kutoa mapendeklezo ambayo yataondoa kasoro zilizokuwepo awali.
Tume ya
Kurekebisha Sheria Tanzania ni Taasisi ya Serikali iliyo chini ya Wizara ya
Katiba na Sheria na ilianzishwa kwa mujibu wa sheria ya Tume ya Kurekebisha
Sheria, Sura ya 171.
Majukumu ya
tume kama yalivyoainishwa katika kifungu cha 4 (1),(2) na (4) Cha sheria ya
Tume ni kufanya mapitio, utafiti na kutathmini maeneo au mfumo wa sheria husika
na kutoa mapendekezo kwa Lengo la kuiboresha.
No comments:
Post a Comment