TANGAZO


Saturday, May 21, 2016

RC PAUL MAKONDA AFUNGUA MACHINJIO YA VINGUNGUTI JIJINI DAR ES SALAAM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto), akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi wakati alipowasili kuzungumza na wafanyabiashara wa nyama katika Machinjio ya Vingunguti kabla ya kuifungua rasmi jana. Katikati ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala,Omari Kumbilamoto ambaye ni Diwani wa Kata ya Vingunguti.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omari Kumbilamoto (wa pili kulia), akielekeza jambo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (wa pili kushoto). Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi na kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Isaya Mngurumi. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Makonda akiongoza ukaguzi huo.
Taswira ya choo cha kisasa kilichojengwa kwenye machinjio hiyo.
Wafanyabiashara katika machinjio hiyo wakimsikiliza Makonda (hayupo pichani).
Mwonekano wa machinjio hiyo baada ya kufanyiwa ukarabati.
Wafanyabiashara wakiwa kwenye mkutano huo wa ufunguzi wa machinji hiyo.
Makonda akisalimiana na wafanyabiashara baada ya kufungua machinjio hiyo.
Wafanyabiashara wakimkabidhi zawadi ya mbuzi Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mngurumi katika hafla hiyo ya ufunguzi wa machinjio hiyo. (Imeandaliwa na Dotto Mwaibale)

No comments:

Post a Comment