TANGAZO


Monday, May 23, 2016

MWEZI APRILI WAVUNJA REKODI YA JOTO KALI ZAIDI DUNIANI

Mwezi Aprili mwaka huu umekuwa mwezi wenye joto zaidi katika historia ya dunia, limesema Shirika la Hali ya Hewa duniani (WMO) katika ripoti yake ya mwishoni mwa wiki (Jumamosi).

Taarifa iliyotolewa na WMO, inaonesha kwamba wastani ya halijoto ya mwezi Aprili imezidi wastani ya karne ya 20 kwa nyuzi 1.1 ya Selisiasi.

Bi. Clare Nullis ni msemaji wa WMO na amesema, "joto tuliloshuhudia mwaka 2015 liligonga vichwa vya habari wakati ule, na tulikuwa na wasiwasi mkubwa." Ameongeza kuwa Joto la mwaka 2016 linaifanya mwaka 2015 kuonekana afadhali.

Amesema sababu ya kwanza ya kuweko joto kubwa zaidi mwaka huu, ni ongezeko la joto duniani na mabadiliko ya tabianchi yaliyosababishwa na mikono ya binadamu.”

Kwa msingi huo Bi. Nullis amesisitizia umuhimu wa kuchukua hatua mara moja za kutekeleza makubaliano ya Paris ili kudhibiti mabadiliko ya tabianchi.

Miji ya Afrika Mashariki kama vile Dar es Salaam, Mombasa na Nairobi imekuwa ikishuhudia joto kali katika miezi ya hivi karibuni na hata katika baadhi ya maeneo kusababisha vifo.

No comments:

Post a Comment