Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Nyerembe Munasa Sabi
akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhus harambee ya kuchangia
ujenzi wa mabweni ya shule ya sekondari Iyunga yaliyoteketea kwa moto hivi karibuni
kulia ni Kaimu Mkurugenzi Jiji la Mbeya Bw.Dkt Samwel Lazaro.(Picha zote na Beatrice Lyimo Maelezo)
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Nyerembe Munasa Sabi
akiongea na waandishi wa habari(Hawapo pichani) kuhus harambee ya kuchangia
ujenzi wa mabweni ya shule ya sekondari Iyunga yaliyoteketea kwa moto hivi
karibuni kulia ni Charles Mwakipesile Mdau wa Maendeleo na kushoto ni Afisa Habari Idara ya Habari Raymond Mushumbusi.
Na Raymond Mushumbusi
MAELEZO
WAZIRI Mkuu
Mhe.Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika harambee itakafanyika
kesho katika ukumbi wa Ubungo Plaza kwa ajili ya kuchangia fedha
zitakazowezesha kukarabati mabweni manne ya shule ya Sekondari ya Ufundi ya Iyunga
yaliyoungua hivi karibuni.
Akizungumza na
waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Nyerembe
Munasa Sabi amesema kuwa wameamua kuomba nguvu kutoka kwa wadau wa elimu na
watanzania kwa ujumla kujumuika katika kuchangia shule ya sekondari ya ufundi
Iyunga ili waweze kukarabati mabweni yaliyoungua kwa moto.
“Hadi sasa takribani
wanafunzi 421 hawana mahala pa kulala kutokana na kuteketea kwa mabweni na kwa
kushirikiana na TAMISEMI tumeamua kusitiza masomo kuanzia tarehe11 March hadi
tarehe 01 Aprili ili kupisha ukarabati wa mabweni.”
“Tumeanza ujenzi wa
baadhi ya miundombinu iliyoteketea na mabweni ikiwa ni jitihada za wadau
mbalimbali waliochangia kutoka Mbeya na nawasihi wanambeya wale waliosoma shule
ya Iyunga na shule za Mbeya na watanzania kwa ujumka kujitokeza kesho katika
harambee hii” Alisema
Mhe. Nyerembe Munasa
Sabi aneongeza kuwa wamepokea michango mbalimbli kutoka kwa wadau wakiwemo Mbeya
Cement waliotoa mifuko 1,000 ya saruji kwa ajili ya ujenzi na kwa sasa mahitaji
yaliyopo ni takribani Shillingi million 770 ili kukarabati na kujenga majengo mapya
kwa ajili ya shule hiyo.
Shule ya Sekondari ya
Ufundi Iyunga yenye wanafunzi takribani
9970 kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita imekumbwa na majanga ya moto
ambayo yamesababisha athari kwa watoto
kutoendelea na masomo na uharibifu wa miundombinu ila Serikali kupitia Tamisemi
na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya wamejipanga kukusanya fedha kwa ajili ya ukarabati mkubwa wa shule
hiyo.

No comments:
Post a Comment