TANGAZO


Monday, March 28, 2016

Watoto wanakufa njaa Somaliland

Image copyrightBBC World Service
Image captionWatoto wamekufa kwa njaa Somaliland
Baa la njaa limesababisha vifo vya watoto na mifugo kufuatia ukame wa miaka miwili Somaliland
Maafisa wa serikali iliyojitangaza huru ya Somaliland wameiambia BBC kuwa hofu imeanza kutanda baada ya mvua kukosa kunyesha kwa mwaka wa pili mfululizo katika maeneo ya Magharibi wa jimbo hilo lililojitenga kutoka kwa jamhuri ya Somalia.
Ali Hamud Djibril amesema kuwa watoto kadhaa wameaga dunia huku maelfu ya mifugo ikifa kufuatia ukame huo uliodumu kwa misimu mwili.
Eneo hilo la Magharibi lilikuwa limewapokea wakimbizi kutoka Ethiopia lakini hali imezidi kuzorota Somaliland.
Umoja wa mataifa unasema kuwa maelfu kwa mamia ya watu wanahitaji msaada wa dharura Somaliland na mashariki mwa Somalia.

No comments:

Post a Comment