Kiongozi wa upinzani ambaye pia ni mwekezaji, Patrick Talon anatarajiwa kushinda uchaguzi wa Urais nchini Benin, baada ya kumshinda Waziri Mkuu Lionel Zinsou.
Matokeo kamili yanatarajiwa kutolewa baadaye leo, Waziri Mkuu Zinsou amempongeza mpinzani wake. Bwana Talon anachukua hatamu ya uongozi kutoka kwa Rais Thomas Boni Yayi ambaye amemaliza mihula miwili.
Uchaguzi Afrika
Katika visiwa vya Cape Verde, chama cha upinzani MPD kimepata viti vingi zaidi vya ubunge. Visiwa hivyo vitafanya Uchaguzi wa Urais baadaye mwaka huu.
Katika nchi za Niger na Congo- Brazaville wapiga kura wanasuburi matokeo ya uchaguzu mkuu. Uchaguzi Afrika
Nchini Senegal matokeo ya kura ya maoni yanatolewa kuhusu marekebisho ya katiba ikiwemo kupunguza muhula wa Rais kutoka miaka saba hadi mitano.
No comments:
Post a Comment