Bofya hapa kwa habari za karibuni zaidi 12:30 Matokeo kamili kama yalivyotangazwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), yanaonesha licha ya Chama cha Wananchi (CUF) kususia, mgombea wake Maalim Seif Sharif Hamad alipata kura 6,076 kwenye uchaguzi wa marudio uliofanyika Jumapili.
Hamad Rashid Mohamed wa chama cha ADC ndiye wa pili akiwa na kura 9,734.
12:20 Mgombea wa CCM Dkt Ali Mohammed Shein amekabidhiwa cheti wa ushindi wa urais.
12:08 Dkt Ali Mohammed Shein atangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais Zanzibar akiwa na kura 299,982.
You need to install Flash Player to play this content.
11:57 Mgombea urais wa CCM Dkt Ali Mohammed Shein yumo ukumbini. 11:54 Bw Jecha kwa sasa anatoa hotuba ya kufungua kikao cha kutangazwa kwa matokeo. 11:49 Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Salim Jecha amewasili ukumbi wa kutangaziwa matokeo. Tume imesema itatangaza matokeo yote muda mfupi ujao. 11:27 Gazeti la Mwananchi linaripoti kwamba mgombea urais wa CCM Dkt Ali Mohamed Shein aongoza matokeo ya awali ya urais majimbo ya Chonga kura 3598, Ziwani (2890), Wawi (4147), Ole (3818), Chake Chake (4551). Matokeo rasmi bado yanasubiriwa. 11:00 Baadhi ya waliowania urais wamefika ukumbini na kuketi. Mmoja wao ni mgombea wa ADC Hamad Rashid. 10:30 Wanahabari, waangalizi na maafisa wengine wa uchaguzi tayari wamo ukumbini wakisubiri kuanza kutangazwa kwa matokeo. 10:20 Kulikuwa na wagombea 14 kwenye karatasi za kura za kumchagua rais. Majina yao ndiyo haya:
1
Khamis Iddi Lila
ACT-W
2
Juma Ali Khatib
ADA-TADEA
3
Hamad Rashid Mohamed
ADC
4
Said Soud Said
AFP
5
Ali Khatib Ali
CCK
6
Ali Mohamed Shein
CCM
7
Mohammed Massoud Rashid
CHAUMMA
8
Seif Sharif Hamad
CUF
9
Taibu Mussa Juma
DM
10
Abdalla Kombo Khamis
DP
11
Kassim Bakar Aly
JAHAZI
12
Seif Ali Iddi
NRA
13
Issa Mohammed Zonga
SAU
14
Hafidh Hassan Suleiman
TLP
10:15 Ulinzi mkali umewekwa
katika ukumbi wa kutangazia matokeo. Mbwa wa ulinzi pia wametumika kukagua eneo hilo, ambalo mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Selim Jecha Selim anatarajiwa kutumia kutangaza matokeo. 10:00 (Saa za Afrika Mashariki). Hujambo! Matokeo ya mapema ya uchaguzi wa marudio uliofanyika visiwani Zanzibar Jumapili yanatarajiwa kutangazwa leo. Karibu kwa taarifa za moja kwa moja kuhusu kutangazwa kwa matokeo hayo.
No comments:
Post a Comment