TANGAZO


Friday, March 25, 2016

Washukiwa sita wakamatwa Brussels

Brussels Polisi wamekuwa wakiwasaka washukiwa wa ugaidi Ubelgiji na Ufaransa

Polisi nchini Ubelgiji wamewakamata washukiwa sita mjini Brussels huku uchunguzi ukiendelea kuhusu mashambulio ya Jumanne yaliyosababisha vifo vya watu 31.
Polisi bado hawajatoa majina yao na pia hawajasema iwapo walihusika katika mashambulio hayo.
Kwingineko Ufaransa, mshukiwa ambaye inasadikika alikuwa akipanga shambulio amekamatwa karibu na mji wa Paris, maafisa wamesema.
Mashambulio hayo ya Brussels yamehusishwa na mashambulio ya Paris ya Novemba mwaka jana.
Kundi linalojiita Islamic State (IS) limekiri kutekeleza mashambulio yote mawili.
Watu waliokamatwa mtaa wa Schaerbeek walikamatwa baadaye Alhamisi, na walinaswa baada ya msako wa nyumba kwa nyumba katika eneo hilo.
Wakazi walisema walisikia milipuko wakati wa msako huo wa polisi lakini chanzo chake hakijabainika.
Jumanne Wakazi wa Brussels wameendelea kuwakumbuka watu waliouawa Jumanne
Aidha, Alhamisi jiobi polisi wa Ufaransa nao walifanya msako katika mtaa wa Argenteuil, kaskazini magharibi mwa Ufaransa baada ya kukamatwa kwa mshukiwa huyo ambaye inadaiwa alikuwa anapanga shambulio
Waziri wa usalama Bernard Cazeneuve alisema mshukiwa huyo, mwenye asili ya Ufaransa, alikuwa kwenye hatua za mwisho za kutekeleza mpango wake, na kuongeza kwamba bado hakujapatikana uhusiano kati yake na mashambulio ya Brussels au ya Paris.
Watu 130 walifariki Novemba mwaka jana baada ya wanamgambo kushambulia maeneo kadha mjini Paris.

No comments:

Post a Comment