TANGAZO


Friday, March 25, 2016

Korea Kaskazini yafanya zoezi la kushambulia makao ya rais

Makao ya rais wa Korea Kusini Park Guen-Hye
Korea Kaskazini imesema kuwa imetekeleza mazoezi ya kuyashambulia makaazi ya rais wa Korea Kusini.
Ni hatua ya hivi karibuni ya ishara za hasira za Pyongyang.
Rais wa Korea Kusini Park Geun-Hye ameliagiza jeshi lake kuwa katika hali ya tahadhari.
Lakini alisema siku ya Alhamisi kwamba uchochezi utasababisha maafa makubwa kwa serikali na uongozi wa Korea Kaskazini.
Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un
Korea Kaskazini imekuwa ikijibu hatua ya Umoja wa Mataifa ya kuiwekea vikwazo kufuatia majaribio ya makombora yake ya masafa marefu ya kinyuklia.
Pyongyang vile vile imekasirishwa na mazoezi ya pamoja kati ya serikali ya Korea Kusini na Marekani kusini mwa mpaka wake.
Kama inavyojulikana kwa vitisho vyake, ripoti hiyo iliyotolewa na KCNA ilitishia kuilipua nyumba hiyo ya rais wa Korea Kusini inayojuliakana kama Blue House hadi kuwa jivu.
Makombora yalirushwa kama umeme na kuanguka katika maeneo yanayolengwa ikiwemo nyumba hiyo ya rais wa Korea Kusini.
Haijulikani ni lini zoezi hilo lilifanywa, lakini ripoti hiyo ilionya mwisho mbaya wa rais Park.
Rais wa Korea Kusini Park Geun Hye
Makaazi hayo ya Blue House yalishambuliwa na makomando wa Korea Kaskazini mwaka 1968.
Hatahivyo jaribio la kutaka kumuua aliyekuwa rais Park Chung-hee halikufanikiwa, raia saba wa Korea Kusini pamoja na makomando hao 31 kutoka Korea Kaskazini waliuawa.

No comments:

Post a Comment